SUPERSPORT KUONYESHA OLYMPIC HADI 2024



Kamati ya Olympic Duniani imeipa tena SuperSport kibali cha kurusha matangazo ya michuano ya Olympic kuanzia mwaka 2018 hadi 2024 barani Africa Kusini mwa jangwa la Sahara.

Makubaliano hayo kati ya kamati hiyo (International Olympic Committee IOC) yanamaanisha kuwa Supersport imepata haki ya kurusha michuano hiyo katika eneo hili la Africa. Michuano hiyo ni pamoja na ile ya  PyeongChang 2018, Tokyo 2020, Beijing 2022 na ile ya mwaka 2024 ambayo bado haijaamuliwa itafanyika katika nchi gani.

Tangazo hilo limetolewa baada ya kukamilika kwa mchakato wa kutoa zabuni kwa warusha matangazo katika kanda hii ya Afrika  - Kusini mwa Sahara. Kwa minajili hii, SuperSport pia itashirikiana na IOC katika kusaidia na kuongeza ufahamu na umaarufu wa michuano hiyo barani Africa.

Rais wa IOC Thomas Bach amekarikiwa akisema: “Tunafurahi sana kufanya kazi tena na DStv SuperSport hususan katika kuwahakikishia wapenzi wa michuano hii fursa ya kuishuhudia popote walipo katika kanda hii ya Afrika – Kusini mwa Sahara. Binafsi nimetembelea nchi mbalimbali barani Afrika na nimeshuhudia ushabiki mkubwa uliopo kwa michuano hii. IOC hutumia asilimia 90 ya mapato yake ya tokanayo na mikataba ya kibiashara katika kuendeleza michezo kote duniani ikiwemo Afrika”.

Naye Gideon Khobane, Afisa Mkuu wa SuperSport amesema  “Sisi tukiwa kama wadau wa muda mrefu na washirika  wa IOC, tumefurahi sana kuingia makubaliano haya na mdau wetu. Michuano hii inawatazamaji wengi sana  kutokana na umaarufu wake na umahiri mkubwa wa kimichezo unaoonyeshwa na hivyo kuwa kivutio kikubwa sana kwa watazamaji. Tunaimani kwa kupitia DStv SuperSport, tunawapa haki mamilioni wa washabiki wa michezo barani Afrika fursa ya kushuhudia michezo ya Olympic, moja ya mashindano makubwa kabisa duniani na yenye msisimko mkubwa”. 

SuperSport ni nguli wa kurusha matangazo ya michezo barani Afrika. SuperSport ina chaneli 37 zinazorusha matangazo ya michezo mbalimbali kuanzia  michezo mikubwa kama vile kandanda pamoja na michezo midogomidogo na ile inayochipukia. Supersport huonekana katika nchi 54 Afrika – kusini mwa sahara pamoja na visiwa vya jirani.

WAKATI HUO HUO Katika kuwahamasisha wateja wake DStv imezindua promosheni maalum ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja wa DStv sasa anaweza kupata fursa ya kujishindia zawadi kemkem ikiwa atalipia king’amuzi chake kwa miezi miwili mfululizo bila kukatika..

Promosheni hiyo itakayoendelea kwa muda wa miezi miwili itatoa washindi wa zawadi mbalimbali ikiwemo vifurushi vya muda wa matangazo, ving’amuzi, pamoja na zawadi kubwa kabisa ambayo ni safari ya kutalii visiwani Zanzibar kwa washindi pamoja na familia zao.

Akielezea promosheni hiyo, Kaimu Meneja wa Uhifadhi Wateja Erick Mosha amesema promosheni hiyo inawalenga wateja wote wenye ving’amuzi vya DStv ambao watakuwa hewani kwa muda wa miezi miwili mfululizo bila kukatika na ni kwa wateja wa vifurushi vyote.

Amesema promosheni hiyo haina ugumu wa kushiriki kwani anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia kifurushi chochote kile cha DStv na kisha kuendelea kutumia huduma hiyo na moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye droo zitakazochezeshwa kila baada ya wiki mbili. Droo ya kwanza itakuwa tarehe 1/08/2017 ikifuatiwa na yapili 15/08/2017 na droo kubwa ya mwisho tarehe 29/08/2017.

Katika droo hizo Zaidi ya washindi zaidi ya 150 watajishindia zawadi mbalimbali huku familia mbili zikipata zawadi kubwa ya safari ya kutalii visiwani Zanzibar. Kila familia itaruhusiwa kuwa na watu wasiozidi wane.

Erick amewataka wateja wa DStv kuchangamkia fursa hiyo ili waendelee kutumia huduma za DStv, kwani kwa sasa kumeongezwa chaneli za kuburudisha na kuvutia zaidi.

“Tunataka wateja wetu wote na Watanzania kwa ujumla wapate fursa nzuri zaidi ya kutumia DStv kwani ndicho king’amuzi kinachoongoza hapa nchini kwa kuwa na chaneli nyingi na zinazopendwa” alisema Erick na kuongeza kuwa kwa sasa wanakaribia msimu wa soka ambapo wale mashabiki wa soka hususan ligi ya Uingereza wataanza tena kushuhudia mtanange huo mubashara kupitia King’amuzi chao cha DStv.

“Tunaendelea kusikiliza maoni ya wateja wetu na kuahakikisha kuwa tunafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuwapatia kile wanachotaka. Mbali na kupunguza bei pia tumeongeza chaneli kwenye vifurushi vyetu na hivi sasa wateja wetu wa kifurushi cha bomba cha Sh 19,975tu, nao wanafurahia ligi kubwa kama Laliga pamoja na baadhi ya mechi za ligi kuu ya Uingereza”


Promosheni ya Jishindie na DStv itafungwa mwisho wa mwezi wa nane ambapo droo kubwa itachezeshwa 29 Agosti.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU