YANGA, SIMBA DUNIA ITASIMAMA KWA MUDA

Wakati Homa ya pambano la Soka la Ngao ya Jamii kwa watani wa Jadi Tanzania, Yanga na Simba ikizidi kupanda kwa kasi kuelekea mchezo huo utakapigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kila upande umejinasibu kushinda kutokana na uimara wa kikosi chake baada ya kila upande kufanya usajili. 

Yanga iliyokuwa ikimsubiri kwa shauku kubwa Kiungo mkabaji Kabamba Thsitshimbi, kutoka Jamhuri ya Congo, imetuliza mzuka baada ya mchezaji huyo kuwasili na kufanya mazoezi pamoja na wenzake walioko Visiwani Pemba. Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa Master amewataka Yanga kutokuwa na hofu na mchezo huo kwani ushindi ni dhahiri kwa Yanga. 

"Hatuna hofu na mchezo huo, tuko vizuri kila idara, tunasubiri siku ya mchezo tuwaonyeshe kazi. Simba wanatamba kupitia vyombo vya habari, Yanga hatuna maneno mengi, waje wamejiandaa kweli maana hatuna mchezo nao", amesema Boniface, mchezaji soka wa zamani, kocha na sasa Katibu Mkuu wa Yanga.

Yanga ambao wamepiga kambi ya maandalizi katika Kisiwa cha Pemba, wameahidi kushinda mchezo huo. huku ikijivunia safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na Donald Dombo Ngoma. Mbali na Ngoma, Yanga ina washambuliaji hatari kama Amis Tambwe, Ibrahimu Ajibu, Obrey Chirwa na Emanuel Martine, Yanga pia inatamba kuwa na kiungo bora upande wa ushambuliaji, Thabani Kamusoko.

Kuwasili kwa Tshitshimbi kumeongeza hamasa katika safu ya ulinzi ya Yanga, ambayo sasa imesheheni mabeki wengi kama, Juma Abdul, Hassan Kessy, Haji Mwinyi, Gaddiel Michael, Nahodha Nadir Haroub 'Canavaro', Kelvin Yondani, Andrew Vicent, Said Makapo na Shaib 'Ninja'. Pia kuna washambuliaji hatari kama Juma Mahadh na Godfrey Mwashiuya, 

Donald Dompo Ngoma. Huyu ni mmoja wa washambuliaji wenye kasi na nguvu katika kikosi cha Yanga, mara kadhaa amekuwa mwiba mchungu kwa Simba.  

 Amis Tambwe, Mara kadhaa ameibuka shujaa katika mchezo wa Yanga na Simba, hususan kutokana na aina yake ya uchezaji. Tambwe anajua mahali goli lilipo kila anapokuwa uwanjani.
 Kiungo Thaban Kamusoko.
 Mshambuliaji Yanga, Obrey Chirwa
 Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina

Wakati Yanga wakitamba kuwa na washambuliaji hao wenye uchu wa magoli. Simba nao wamejinasibu kuwa Yanga lazima wafe kwa idadi kubwa ya mgoli, huku wakijivunia washambuliaji wake hatari kama Emanuel Okwi, John Boko, Shiza Ramadhan Kichuya na Kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima. 

Shabiki nazi wa timu hiyo, ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Aden Ismail Rage, amekaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa Yanga hakuna mchezaji wa kuzuia Okwi, Boko na majaro za Niyonzima zinaleta raha. Rage amesema angekuwa kiongozi wa Yanga angesema wazee chukueni tu hiyo ngao ya jamii maana Yanga wamekoswa sana goli saba.

"Ningekuwa kiongozi wa Yanga ningesema wazee hiyo Ngao ya Hisani chukueni tu maana wakitia mguu saba, hakuna wa kumzuia Okwi, hakuna wa kumzuia Boko, na kros za Niyonzima zinaleta raha", amesema Rage kupitia mitandao ya kijamii.

Naye msemaji wa Simba, Haji Manara amesema iwapo Simba itafungwa na Yanga yeye ataihama timu hiyo, lakini hakusema atahamia upande gani. "Hatufungwi, hatufungwi, hatufungwi, tukifungwa mimi nitahama Simba", amasisitiza Manara.

 Mshambuliaji tegemeo wa Simba, Emanuel Okwi, ambaye mashabiki wa timu hiyo wanamtegemea kwa asilimia mia kuifunga Yanga katika mchezo wa ngao ya hisani Jumatano.
 John Boko wa Simba
 Shiza Kichuya na Mavuigo
Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU