Mhubiri
wa Kimataifa Prophet Nicolaus Suguye (pichani), wa Kanisa la Huduma ya The Word of
Reconciliation Ministries (WRM), lenye Makao Makuu yake Kivule Matembele ya pili Jijini Dar es Salaam, akishirikiana na vingozi
mbalimbali wa kiroho watafanya maombi maalum ya kuliombea Taifa Tanzania na viongozi wake, ili Mungu awaepushe na mabaya yote, ili kuwe na upendo amani na utulivu uzidi kudumu kwa ustawi wa jamii na taifa kwa
ujumla.
Tukio hilo maalumu linatalajiwa kutafanyika katika mkutano mkubwa wa injili, utakaohudhuriwa na watu wa dini zote na madhehebu yote kutoka ndani na nje ya nchi, utafanyika katika viwanja vya Hali ya hewa, vilivyoko Banana, Ukonga Dar es Salaam, kuanzia Septemba 27 hadi Octoba Mosi mwaka huu.
Kwa mjibu wa Nabii Saguye, watu wenye shida mbalimbali wataombewa. Mtumishi huyo wa Mungu, aliyabainisha hayo katika mahojiano maalum na Mwandishi Maalumu, alipotaka kujua kwa jinsi gani viongozi wa dini wanaunga mkono juu za serikali katika kuwaletea maendeleo ya wananchi. Nabii Saguye alisema kuwa huduma yake imekuwa mstari wa mbelee katika kusaidiana serikali katika suala zima la kuwaletea wananchi maandeleo na kuongeza ajira kupitia Nyanja tofauti ikiwemo vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Huduma hiyo.
‘’Tumekuwa tukifanya mambo mengi ya kimaendeleo lakini pia tumekuwa tukifunga na kuwambea viongozi wetu ili Mungu azidi kuwatia nguvu katika kuwatumikia wananchi.Ttunathamini sana kazi wanayoifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo bila ubaguzi wowote.
Nabii Saguye amesema viongozi wa kiroho wana jukumu la kuombea nchi na serikali ili Mungu azidi kushusha neema na nguvu, kuwaepusha na hila mabaya katika kufanya kazi ya nchi ambayo ni kuwatumikia wananchi. Amesema wameandaa mkutano mkubwa wa njili hapa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuombea viongozi wa nchi na kumuomba Mungu, amani na utulivu tuliyonao uendelee kudumu.
Amesema wanaunga mkono kazi Nzuri sana na iliyotukuka inayofanywa na Mheshimiwa Rais wa Awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli. "Rais Magufuli amedhamilia kuwaletea watanzania maendeleo ya kweli’’ amesema Nabii Prophet Suguye
Aidha alisisitiza kuwa mbali na kuliombea taifa kutakuwa na maambezi maalum kwa ajili ya watu wote watakaohudhuria Mkutano huo na wenye shida mbalimbali na wanasumbuliwa na majini na nguvu za giza watafunguliwa na kuwekwa huru baada ya maombezi hayo.
Taarifa zinasema Mkutano huo wa Injili wa siku tano unategemewa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiroho na serikali kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania na utakuwa wa madhehebu yote na dini zote bila ubaguzi wowote wa kiimani wala kidini.

Nabii Prophet Nicolaus Suguye akipiga goti wakati wa maombi
Nabii Prophet Nicolaus Suguye akiwaombea wananchi
Naboii Prophet Nicolaus Suguye akisoma Biblia.
Nabii Prophet Nicolaus Suguye akihubiri neno la uzima
Comments
Post a Comment