HEKAYA ZA ABUNUWASI
HEKAYA ZA ABUNUWASI ni kitabu cha hadithi za kusisimua, zinazofurahisha sana kutokana na umahili wa watunzi wa vitabu vya kale. Kutokana na utamu wa hadithi za ABUNUWASI, Blog ya MPIGANAJI itawaletea hadithi hizo ili kuwachangamsha akili............... KISA CHA ABUNUWASI NA MFALME SIKU moja alfajiri, wakati wananchi wa mji wenye wakazi wengi walipokwenda kuchota maji mtoni, walishangazwa kuuona mkono wa mtu ukiwa katikati ya mto. Mkono huo wa ajabu ulikuwa umenyoosha vidole viwili juu, kuonyesha alama ya mbili. Wananchi walistushwa sana na kitendo hicho, wakaogopa hata kuchota maji mtoni, kwani hawakuwahi kuona tukio la kuogopesha kama lile. Wengine waliamini kuwa huo ulikuwa mwili wa mtu aliyetupwa mtoni. Lakini ishara iliyoonyeshwa na mkono huo iliwafanya wananchi waamini kuwa huo ulikuwa mkono wa ajabu. Katika kiza kinene kilichozunguka ndani ya vichwa vya wananchi, habari zikamfikia Mfalme wao, naye akafika haraka eneo la tukio. Mfalme wa nchi hiyo baada ya kujiridhisha k...
Comments
Post a Comment