Kizazaa, baada ya wafanyabiashara wa mafuta kugoma kutoa huduma hiyo kwa visingizio vya kushuka kwa bei, Jijini Dar es Salaam, kumesababisha kituo pekee kilichouza mafuta cha TSN, kando ya Barabara ya Bagamoyo, eneo la Bamaga, kufurika magari Dar es Salaam leo yakisubiri kupata mafuta.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inapenda kutoa taarifa juu ya kinachoendelea katika sekta ndogo ya mafuta, ambapo vituo vingi vimeonekana kukosa mafuta ya petroli.
Kwanza nchi ina mafuta ya kutosha kwa siku 33 kulingana na aina ya mafuta kwa maana kwamba petroli, ipo ya siku 33, dizeli siku 32 na mafuta ya taa yapo ya siku 38. Kwa siku tunatumia lita 875,000 za petroli, 3,100,000 za dizeli na lita 615, 240 za mafuta ya taa.
NINI KILICHOJITOKEZA
Katika mfumo wa biashara ya mafuta hapa nchini kuna wafanyabiashra wa aina mbili; wale wanaomiliki vituo na magala (Company Owened, Company Operated –COCO) na wale wanaomiliki kituo kimoja kimoja na hawana uhusiano kabisa na wenye maghala na wala hawana magala ya mafuta (Dealers Owned, Delaers Operated-DODO).
Kutokana na kushuka kwa bei za mafuta, hususani petroli kwa shilingi 108 kwa lita, 99 kwa dizeli na 91 kwa mafuta ya taa, kushuka ambako ni kukubwa sana, DODO wengi ambao ni vituo vingi na mitaji yao ni midogo wanaangalia kwanza bei kikomo zinazotolewa na EWURA zina mwelekeo upi ndio wakanunue kwenye magahala ya mafuta.
Kwa bahati mbaya bei hizi zinaanza Jumatatu hivyo, Jumatatu inatumika kununua mafuta kutoka kwenye maghala. Hii inatokana na ukweli kwamba hakuna mtu ambaye (DODO) anayeweza kuthubutu kubaki na akiba ya mafuta kubwa katika kipindi hiki ambapo bei za mafuta zinashuka kwani ataingia katika hasara kubwa.
Hivyo, basi pamoja na changamoto zilizopo ni matarajio yetu kuwa biasahara hii itatengemaa kuanzia kesho Jumanne.
KUTHIBITISHA KUTENGEMAA KWA BIASHARA
Hadi leo, Desember 19, 2011 upakiaji wa mafuta ulifikia au kuzidi matumizi ya kila siku kwa maana kwamba petrol, ilipakiliwa lita 1,434,950, dizeli 2,948,000 na mafuta ya taa ni lita 600,000 na uuzwaji wa mafuta ulikuwa unaendelea.
Hata hivyo, EWURA itaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama kuna vituo vina mafuta lakini haviuzi ili adhabu stahiki ichukuliwa.
USHAURI
EWURA Kama mdhibiti anashauri kuwa ni yeye pekee ambayea anaweza kutamka mafuta hakuna, hivyo basi hakuna haja kwa umma kupata hofu na kuanza kujazana kwenye vituo vya mafuta kujaza mafuta zaidi ya idadi ya lita mabazo mara nyingi hujazwa kwani kwa kufanya hivyo, kunaharibu mfumo mzima wa usambazaji wa mafuta.
EWURA Kama mdhibiti anashauri kuwa ni yeye pekee ambayea anaweza kutamka mafuta hakuna, hivyo basi hakuna haja kwa umma kupata hofu na kuanza kujazana kwenye vituo vya mafuta kujaza mafuta zaidi ya idadi ya lita mabazo mara nyingi hujazwa kwani kwa kufanya hivyo, kunaharibu mfumo mzima wa usambazaji wa mafuta.
NINI CHA KUFANYA
EWURA inaharakisha marekebisho ya Kanuni ambayo itafanya utoaji wa bei za mafuta ubadilike kutoka siku 14 za sasa kama ilivyo kwenye Sheria ya sasa kwa mujibu wa Gazeti la Serikali ili kukabiliana na upungufu wa mafuta unaotokana na bei mpya kutoka Jumatatu.
Comments
Post a Comment