WAZIRI MKUU ALIYEJIUZULU EDWARD LOWASA
HIVI karibuni baadhi ya vyombo vya habari vya ndani ya nchi, vilimkariri Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhwan Kikwete, ambaye pia ni mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, akiwataja Makada 11 wa Chama Cha Mapinduzi wanaofaa kuvaa viatu vya baba yake.
Miongoni mwa wanasiasa waliotajwa na Ridhawan kuwa wana sifa za kuvaa viatu vya JK, yumo Mwana mama mmoja tu, ambaye ni Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Asha Rose Migiro, aliyewahi pia kuwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa (UN), pia ni Mbunge wa kuteuliwa na Rais. Hata hivyo Migiro anatajwa kuwa hana ushawishi kabisa wa kushika wadhifa huo mkubwa nchini.
Wengine ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa Uratibu na Mahusiano, Bw. Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba na Mbunge wa Songea, Dkt. Emanuel Nchimbi.
Ridhwani aliwataja makada wengine kuwa Mbunge wa Sengerema, William Ngereja, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddy, ambao pia wanatajwa na duru za kisiasa kuwa hawajakomaa kushika wadhifa huo w rais wa Taifa kubwa lenye heshima kama Tanzania.
Kama Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere alivyowahi kusema, Urais ni mzigo mzito, kwa mtu safi kabisa hawezi kukimbilia Ikulu. Pia akasema ukimuona mtu anapenda sana kwenda Ikulu, huku akihonga pesa, huyo hafai kuingia Ikulu, huku akisisitiza Ikulu kuna biashara gani hata mtu anahonga ili aende Ikulu. Hayo ni maneno ya Mwalimu Nyerere tuliyempenda sana.
Katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa tano wa vyama vingi nchini Tanzania mwaka 2015, msuguano mkali umeibuuka miongoni mwa wanasiasa wanaousaka urais wa Tanzania kwa udi na uvumba, huku wengine wakitishia kutoa roho za watanzania mradi tu wapate kuitwa Mheshimiwa rais.
Kwenye vijiwe vya kuuzia magazeti na sehemu kadhaa zenye mikusanyiko mikubwa ya wananchi, hususan waliosoma ama kusikia kuhusu majina ya watanzania wanaofaa kuvaa viatu vya JK, baadhi walitoa ya moyoni mwao huku asilimia kubwa wakimtaja Edward Lowassa kuwa ndiye anafaa kuendesha jahazi.
Kwenye gazeti la Mwananchi toleo la jana, July 15, 2014, kulikuwa na picha saba zilizoambatanishwa pamoja na majina yao, Lowasa akiwa miongoni mwa wanasiasa wanaotajwa kuwania urais 2015, tofauti na matarajio ya wengi, karibu kila mmoja alionyesha hisia zake kwa Edward Lowasa, kama wanavyosema.
ABDUL MHEMBANO WA MBAGALA; "Kati ya hawa wote mimi kwa upande wangu namkubali huyu", anasema huku akionyesha picha cha Lowasa kwa kidole. Alipoulizwa sababu za kumpenda Lowasa, Abdul anasema, Lowasa ni kiongozi mwenye msimamo usioyumbishwa, ambayo ni sifa mojawapo ya kuwa rais.
SAMWEL KITNDU WA YOMBO; "Ndani ya CCM sijaona kiongozi wa mfano wa Lowasa, huyu mimi namfananisha na hayati Edward Moringe Sokoine, nakumbuka wakati akiwa Waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu, alikuwa halali, kila siku utamsikia Lowasa yuko huku au huku akitekeleza majuku yake kama Mtendaji Mkuu wa Serikali, siku hizi Waziri hata simsikii hivi yupo?", anahoji Samwel.
MUSSA MKATI WA KIMARA; "Lowasa peke yake anaweza kurejesha heshima ya taifa kama alivyofanya Hayati Sokoine, alipokuwa Waziri Mkuu wakati wa Serikali ya Awamu ya kwanza ya Hayati Mwalimu Nyerere, hakumuonea mtu na hakupenda wananchi waumizwe na ufisadi, hakuna anayejuwa kuwa Sokoine ndiye aliyetangaza vita dhidi ya Wahujumu Uchumi na Walanguzi, ni vita ngumu lakini ina faida kwa watanzania wengi", anasema Mussa.
Lowasa ambaye amewahi kuishika nyadhifa mbali mbali serikalini kuanzia utawala wa Serikali ya awamu ya pili ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, kama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kuu, Waziri wa Maji, Waziri wa Mifugo na hatimaye Waziri Mkuu, alikuwa msaada na swahiba mkubwa wa Rais Kikwete, wakati huo wakiitwa TWO BOYS MEN.
Kutoka na hali hiyo, kwa mtazamo wangu binafsi bila kuwashinikiza watanzania wengine kukubaliana na hili, NATHIBITISHA KUWA SIJAMUONA KIONGOZI MADHUBUTI NDANI YA CCM WA KUSHINDANA NA EDWARD NGOYAY LOWASA. Tuombee uchaguzi Mkuu 2015 uwe wa amani na upendo utawale kwa watanzania wote tupate kiongozi makini.
MBUNGE WA MONDULI KWA TIKETI YA CCM EDWARD LOWASA
MBUNGE WA CHALINZE, RIDHWAN KIKWTE AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI KUHUSU MAKADA WA CCM WANAOFAA KUVAA VIATU VYA BABA YAKE.
Comments
Post a Comment