Mke wa Rais
wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela, Bi. Graca Machel ambaye ni Mwanaharakati
wa Haki za Binadamu, akisalimiana na Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria, Bi. Angellah Kairuki, Dar es Salaam jana, alipofika kuunga mkono jitihada za kukomesha vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni. Wengine ni wadau kutoka Wizara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)
Bi. Graca Machel (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuunga mkono
juhudi za kupambana na vitendo vya ukeketaji na ndoa za
utotoni. Kushoto ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Angellah Kairuki na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
idadi ya watu Duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Natalia Kanem.
Comments
Post a Comment