Meneja Uhifadhi wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo (wa pili kulia) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya Jishindie na DStv iliyofanyika katika ofisi za Multichoice Tanzania Dar es Salaam jana. Wengine ni Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Ronald Shelukindo (kushoto) Meneja Operesheni wa Multichoice Abdalla Hemed na Erick Mosha wa kitengo cha Uhifadhi wateja. Takriban washindi 200 wameshinda zawadi mbalimbali kwenye promosheni hiyo ikiwemo safari ya kutalii Zanzibar kwa familia mbili.
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo (katikati) akifurahia jambo na Mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha Abdallah Hemed (Kushoto) na Afisa wa uhifadhi wateja wa Multichoice Tanzania Erick Mosha wakati wa droo ya promosheni ya Jishindie na DStv iliyofanyika jana katika ofisi za Multichoice Tanzania Dar es Salaam.
JIJINI Dar es Salaam jana Jumanne Septemba 5, 2017; Wateja 76 wa DStv wamejinyakulia zawadi mbalimbali kutoka Multichoice Tanzania katika droo kubwa ya promosheni ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja wa DStv anapata fursa ya kujishindia zawadi kwa kulipia king’amuzi chake kwa angalau miezi miwili mfululizo.
Kati ya washindi hao 25 wamejipatia zawadi ya ving’amuzi vya DStv Explora ambavyo ni ving’amuzi vya kisasa kuliko vyote hapa nchini. Washindi wawili wamejishindia Kifurushi cha Premium cha Tsh 169,000) cha mwezi, wengine wawili Kifurushi cha Compact+ cha Tsh 109 000), huku washindi 10 wakishinda kifurushi cha Compact cha Tsh 69,000), 10 kifurushi cha Famili (39,000) na wengine 25 Kifurushi cha Bomba cha Tsh 19,000.
Washindi wawili wa droo kubwa ambao ni Anicet Macheta waKagera na Hassan Juma Hassan wa Dar es Salaam wamejishindia zawadi kubwa kabisa ambayo ni safari ya kutalii visiwani Zanzibar wao pamoja na familia zao zisizozidi watu wane kila familia.
Akizungumza baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ya mwisho leo hii katika ofisi za Multichoiche Tanzania, Meneja wa Uhifadhi Wateja Hilda Nakajumo amebainisha kuwa zaidi ya wateja 30,000 wameshiriki kwenye promosheni hiyo iliyoendelea kwa miezi miwili.
Hilda amesema, wamefurahi kuona kuwa washindi takriban 200 waliopatikana wakati wote wa promosheni wametoka maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo Arusha, Mwanza Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Ruvuma na mikoa mingine kote nchini.
“Wakati wote DStv tunahakikisha kuwa wateja wetu wanafurahia huduma zetu kwani mbali na kwamba sisi ni vinara katika burudani na michezo, pia tunakuwa na promosheni za mara kwa mara ambapo wateja wetu hupata zawadi mbalimbali” alisema Hilda.
Amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa neema kwa wateja wa DStv kwani mbali na kuongeza chaneli kwenye vifurushi hususani vile vya bei ya chini, pia hivi majuzi DStv ilipunguza bei za vifurushi vyake vyote ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata huduma hizo kwa unafuu mkubwa.
Kampuni ya Multichoice Tanzania inayoendesha biashara ya vingamuzi vya DStv, ina umri wa miaka 20 sasa ambapo ilianza shughuli zake hapa nchini mnamo mwaka 1997.
Comments
Post a Comment