Dar es Salaam; Kwa mara nyingine DStv kupitia Channel yake ya Maisha Magic Bongo (MMB) inaleta mapinduzi katika Tasnia ya Filamu nchini kwa kuongeza tamthilia nyingine mbili ili kuwahakikishia watanzania na wateja wa DStv burudani zaidi.
Tamthilia hizi mpya ni SARAFU na KAPUNI ambazo zimezinduliwa na Waziri ha Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dr. Harison Mwakyembe pamoja na maafisa mbalimbali wa wadau wa Tasnia ya Filamu nchini katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam zitaanza kurushwa hewani kuanzia wiki ijayo katika DStv channel 160 – Maisha Magic Bongo.
Akielezea kuhusu tamthilia hizo mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande amesema KAPUNI ni Tamthilia iliyoandaliwa na Mtanzania Leah Mwendamseke na imesheheni vituko na misukosuko ya mahusiano, usaliti wa kimapenzi unaoleta chuki, uhasama na uadui mkubwa lakini cha kushangaza ni mapenzi hayo hayo yanayoleta suluhu kati ya pande mbili zinazogombana.
Amesema tamthilia hii imeigizwa na waigizaji maarufu kama Jacquline Wolper, Gabo, Kajala, Masanja, Jenifer Kyaka (Odama), Mwanamuziki Quick Rocka, DJ maarufu Rommy Jones na mastaa wengine wengi.
Maharage amebainisha kuwa tamthilia ya SARAFU iliyoandaliwa na John Samwel Isike, nayo ni tamthilia maridadi iliyobeba marafiki wawili ambao wanaingia kwenye chuki na uadui mkubwa mpaka kuingiza familia zao kwenye hatari kisa ni fedha zinazozaa kiburi dharau na anasa za kupitiliza. Waigizaji maarufu akiwemo Mohammed Funga Funga ( Mzee Jengua), Mzee Chilo, Elizabeth Michael (Lulu), Hemed Suleiman, Irene Uwoya, Idris Sultan, Yusuph Mlela na mastaa wengineo wamo kwenye tamthilia hii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Mwakyembe amewataka wasanii hapa nchini kuhakikisha kuwa wananufaika na kazi zao za Sanaa na kwamba serikali na yeye binafsi kwa dhamana aliyonayo wako tayari muda wote kushirikiana na wasanii kuhakikisha wanapata haki zao kutokana na kazi zao.
Amesema amefurahishwa sana na kiwango cha hali ya juu kilichoonyeshwa katika tamthilia hizo mpya ambazo zote zemebuniwa na kutengenezwa hapa nchini na waigizaji wake, wahariri na waongozaji wote ni watanzania.
Pia amewaasa wasanii kuhakikisha kuwa wanazingatia maadili ya jamii yetu wakati wote wanapofanya kazi zao za Sanaa kwani Sanaa ni kioo cha jamii na kwamba ikitumika vibaya inaweza kuwa na athari mbaya kwa jamii yetu.
Tamthiliaya KAPUNI itaanza kurushwa hewani kuanzia Januari 8, 2018 kupitia DStv 160 - Maisha Magic Bongo kila siku za Jumatatu na Jumanne saa 1:30 Jioni wakati ambapo ile ya SARAFU itaanza kwenda hewani kuanzia Januari10, 2018 kila siku ya Jumatano na Alhamisi saa 1:30 jioni. Mzunguko wa kwanza wa tamthilia hizi unatarajiwa kuendelea hadi mwezi Machi 2018.
DStv kupitia chaneli yake mahsusi ya maudhiu ya Kitanzania ya Maisha Magic Bongo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa tasnia ya Sanaa inakua na kuifanya iwe moja ya vyanzo muhimu vya mapato kwa wasanii na hatimaye kuchangia katika uchumi wan chi yetu.
Chanel ya Maisha Magic Bongo ilianzishawa tarehe 1 Octoba 2015, kwa lengo kuu la kuinua na kukuza vipaji na Sanaa hapa Tanzania na pia kuongeza maudhui ya kitanzania kwa wateja wa DStv.
Kwa kipindi chote hiki Channel hii imekuwa kwa haraka sana ambapo kwa sasa ni miongoni mwa Channel zenye watazamaji wengi Zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Channel hii imekuwa kitovu cha maendeleo ya wasanii hapa nchini huku mamia ya wasanii wakipata fursa mbalimbali kutokana na kazi zao kurushwa katika channel hii na pia kupata mafuzo na kipato kupitia Sanaa.
Kwa upande wa tasnia ya filamu na uigizaji, Maisha Magic Bongo imeleta mapinduzi makubwa na miongoni mwa filamu zinazotikisa katika soko kwa sasa ni pamoja na Tamthila ya HUBA,ambayo ilipokelewa vizuri sana na Watanzania, pia kuna filamu na vipindi vingine kama MWANTUMU, HARUSI YETU, KITIMTIM ambazo zote zinazidi kuwa maarufu kila uchao.
Kuingizwa kwa tamthilia mpya za Kapuni na Sarafu, nu muendelezo wa mkakati wa Chaneli hii kuongeza maudhui ya kitanzania, na kuwapa watanzania burudani inayoendana na wakati na yenye kuakisi maisha halisi ya kitanzania.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harishon Mwakyembe(katikati) na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisoo (Kulia) wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande muda mfupi kabla ya uzinduzi rasmi wa tamthilia mbili mpya za Kitanzania – SARAFU na KAPUNIzitakazoonikana katika chanel ya Maisha Magic Bongo kuanzia mwezi huu. Tamthilia hizo zimeigizwa na wasanii maarufu kama Jacquline Wolper, Gabo, Kajala, Mwanamuziki Quick Rocka, Mohammed Funga Funga (Mzee Jengua), Irene Uwoya, Idris Sultan na wengineo.
Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni a Michezo Dkt. Harishon Mwakyembe na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisoo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande (kushoto) na Mbunge wa Makete Prof. Norman Sigalla King wakifuatilia kwa makini tamthilia mpya za Kitanzania – SARAFU na KAPUNI zitakazoonikana katika chanel ya Maisha Magic Bongo kuanzia mwezi huu. Tamthilia hizo ambazo zimezinduliwa rasmi jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam zimeigizwa na wasanii maarufu kama Jacquline Wolper, Gabo, Kajala, Mwanamuziki Quick Rocka, Mohammed Funga Funga ( Mzee Jengua), Irene Uwoya, Idris Sultan na wengineo.
Wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu nchini wakifuatilia kwa makini tamthilia mpya za Kitanzania – SARAFU na KAPUNI zitakazoonekana katika chanel ya Maisha Magic Bongo kuanzia mwezi huu wakati wa uzinduzi wa tamthilia hizo jana katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Tamthilia hizo zimeigizwa na wasanii maarufu kama Jacquline Wolper, Gabo, Kajala, Mwanamuziki Quick Rocka, Mohammed Funga Funga ( Mzee Jengua), Irene Uwoya, Idris Sultan na wengineo.
Comments
Post a Comment