Miaka 32 ya Vita vya Kagera na ushindi wa Majeshi ya Tanzania

Watanzania walivyojifunga vibwebwe kuitetea Kagera
*Kipigo cha Lukaya kiliweka historia ya ushindi

Mnamo mwaka 1978, majeshi dhalimu ya Nduli Idi Amin wa Uganga yalivamia Ardhi ya Tanzania, eneo la Mto Kagera, mkoa wa Ziwa Magharibi na kufanya uharibifu mkubwa wa mali na maisha ya wananchi wa mkoa huo, kama Mwandishi Wetu NYAKASAGANI MASENZA anavyosimulia kupitia vyanzo mbali mbali vya habari.

Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika suala zima ukombozi wa Bara la Afrika, ikiwa miongoni mwa mataifa masikini zaidi duniani, lakini lililojariwa kuwa na viongozi shupavu wenye hekima na busara.

Muasisi wa kwanza wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere, alionesha njia kwa kuachia uongozi kwa hiari yake mwenyewe na Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi alipewa nafais ya kuongoza jahazi, akifuatiwa na Benjamin Mkapa na hatimaye Jakaya Kikwete.

Busara za viongozi wa Tanzania zilianza kuonekana mwaka 1961, Mwalimu Nyerere alipowatoa watanzania kutoka kwenye mikono ya wakoloni, wakati huo pia akiwa tayari hata kuchelewa kupandisha bendera ya Uhuru wa Tanganyika, ili nchi zingine za Kiafrika kama Kenya na Uganda zilizokuwa kwenye mchakato wa kupata uhuru ziungane na Tanzania kupata Uhuru siku moja.

Msimamo Mwalimu Nyerere usioyumbishwa, ulijenga Tanzania imara na kuifanya kuwa kimbilio la vikundi vya wapigania uhuru Kusini mwa Afrika, ambao walipewa kambi na hifadhi za kudumu na kuruhusiwa kutumia ardhi ya Tanzania kama sehemu ya mapambano ya kudai uhuru, ambao hatimaye waliupata kupitia mgongo wa Tanzania.

Miongoni mwa nchi zilizoweka kambi Tanzania wakati wa kudai uhuru ni Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini na nyinginezo nyingi. Baadhi ya nchi hizo zina uchumi mzuri sasa.

Watanzania walianza kuingiwa na wasiwasi mwaka 1971, wakati Nduli Idi Amin Dada alivyoasi na kuchukuwa madaraka ya Uganda kwa nguvu baada kuungusha utawala halali wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Hayati Milton Obote na kutangaza kuitawala nchi hiyo kijeshi.

Mwanzo wa utawala wake waganda pamoja na mataifa mengine walidanganyika, wakawa na matumaini makubwa juu ya kiongozi huyo wa kijeshi, kutokana na ahadi zake nyingi kwamba yeye ataitala uganda na kuhakikisha eneo lililoko Tanzania, sehemu ya mto kagera, katika mkoa wa Ziwa Magharibi litakuwa sehemu ya Uganda.

Mwaka huo huo, Idi Amin alijaribu kutimiza madai yake kwa kuishambulia sehemu hiyo ya Mto Kagera, lakini watanzania walikuwa imara katika kulinda ardhi yao sehemu hiyo akashindwa, baada ya majeshi yake kurudishwa nyuma na majeshi hodari ya Tanzania.

Pamoja na majeshi yake kurudishwa nyuma, Fashiti huyo aliyejitangaza kuwa Rais wa maisha wa Uganda, akiwapongeza wapiganaji wake kwa kurudishwa nyuma huku akiwasifia kupata jeraha kidogo kutoka kwa majeshi ya Tanzania.

Baada ya wapiganaji wake kurudishwa nyuma Idi Amin alisema huo ni mwanzo tu, awamu nyingine atatumia silaha nzito zaidi ikiwa pamoja na makombola ya kurushwa kwa ndege na kuwaongezea nguvu askari wa miguu, jambo ambalo liliwafanya waganda kuingiwa na hofu kutokana na utawala huo wa mabavu, baada ya Amin kuanza kuwatilia shaka wananchi na kuwaua hovyo.

Mauaji ya kinyama yakawa kitu cha kawaida katika Uganda, wananchi wengi wasiokuwa na hatia walipoteza maisha, watu mashuhuri kama Jaji Mkuu Benedicti Kiwanuka na Askofu Mkuu Jamal Luwumu, waliteswa na kuuawa chini ya utawala wake.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU