NJAMA
SURA YA TATU
VERONIKA NA SHERRIFF

Asubuhi hii niliamka mapema, na baada ya kuoga na kuvaa vizuri niliamua nikastaftahi hapo Palm Beach Hoteli, kwani niliona uvivu kujipikia chai. Kama kuna kitu nachukua ni mambo ya kupikapika.

Nilikuwa mtu wa kwanza kufika Palm Beach Hoteli kwa ajili ya kusitaftahi. Kijana mmoja muuza magazeti alinifuata ndani ya chumba cha chakula na kuniuzia magazeti ya Daily News na Uhuru. Nilipitisha macho kwenye magazeti haya huku nikisubiri niletewe chemsha kinywa.

Magazeti haya yalijaa habari nyingi kama kawaida, lakini habari juu ya tukio lililokuwa limetokea katika wiki hii haikuwemo. Bila shaka ilikuwa imeachwa kwa ajili ya usalama. Nilipoletewa chemsha kinywa niliishambulia haraka haraka, nikalipa na kuondoka kuelekea ofinini. Wakati huo ilikuwa yapata saa moja na nusu.

Nilipokuwa napita karibu na nyumba yangu, mara akili ikanijia kuwa afadhali nichukua bastola yangu kwani nisingeweza kuamini tu kuwa hali ilikuwa ya usalama. Nilirudi nyumbani kwangu, nikachukua bastola moja aina ya 38mm ya kipolisi na kuiweka ndani ya shati langu kwa jinsi ambavyo isingeweza kuonekana kwa urahisi.

Nilichomeka shati vizuri, nikafunga mkanda wa suruali na kuifungia vizuri bastola chini kidogo ya kitovu. Kwa sababu kulikuwa na hali ya mawingu-mawingu nilivaa jaketi juu. Kisha nikaelekea ofisini.

Nilikuta ofisi imeshafunguliwa, nikapita nikawasalimia maofisa wangu wadogo, kisha nikaelekea ofisini kwangu. Linda alikuwa tayari ameshafika.

"Hallo bosi, umelalaje?", Linda alinisalimia nilipofungua mlango na kuingia ndani.

"Safi kabisa, je wee?".

"Mimi ndiye nimelala vizuri kabisa, hata sikuota leo ingawaje mimi ni muotaji".

"Itabidi uwe unalala si chini ya masaa sita, bado mtoto mdogo wewe".

"Sawa, lakini panapokuwa na shughuli maalum sina budi kukesha.

"Kama ndivyo hivyo naona kazi itafanyika".

"Na usiwe na shaka, itafanyika".

"Niitie Eddy aje ofisini kwangu".

"Sawa bosi".

Kwa sababu Namba mbili, tatu na namba nne walikuwa safarini huko Kusini mwa Afrika kwa shughuli maalum, ilibidi katika shughuli hii nishirikiane na kijana Eddy Kisanga, ambaye alijitokeza kuwa kijana shupavu sana katika kazi yetu hii.

Eddy alikuwa kijana mwenye umri wa miaka ishirini na mitatu, lakini alikuwa na akili za kuweza kumiliki matatizo na kujifunza mambo magumu katika kazi yetu hii kwa haraka sana.

Kitu cha kutufurahisha ni kwamba alikuwa mwanafunzi wangu mimi mwenyewe, hivyo matendo yake yalifanana na yangu, kiasi kuwa hapa ofisini aliitwa Willy mtoto.Na yeye alikuwa akifurahi sana kuitwa hivyo.Kwa hiyo nilipopeleka jina lake kwenye kamati ya upelelezi, nikawa nimeweka sifa zake kama mimi haikuwa ajabu kukuta amethibitishwa.

Baada ya kuthibitishwa ilibidi apewe kazi maaum ili kumpima na kuweza kumpa namba. Hivyo yeye na Sammy Rashid namba mbili walikuwa kwenye kazi maalum huko Johannesburg, Afrika Kusini. Kazi hiyo ilitekelezwa vizuri sana, na waliporudi namba mbili alitoa ripoti juu ya kazi hiyo na ikaonekana sehemu aliyofanya Eddy ilimshangaza hata Chifu, Eddy aipewa namba ya juu kuiko wote tuivyotegemea na kutokana na muda wake kazini; Kutoka kwenye kamati ya usalama alipewa namba 'TANO'.

"Eddy yuko hapa", Linda ainieleza kwa simu.

"Mwambie aingie", nilimjibu.

Eddy aiingia ndani nikamuonesha kwa ishara ya mkono avute kiti aketi.

"Habari za leo bosi", alisalimia Eddy.

"Nzuri, habari yako wewe?".

"Ni nzuri".

"Eddy natumaini umesikia jambo lililotokea hapa mjini siku chache zilizopita?".

"Ndio, lakini nimezisikia kwenye radio za nje, na rafiki yangu mmoja polisi wa kituo cha kati, ndiye aiyenielezea kwa kirefu kidogo. Vile vile alinieleza kuwa wao ndio wanapeleleza tukio hili lakini kufikia sasa hawajafika popote. Wanasema mpaka sasa hawajaona au kupata kitu chochote kinachohusika na tukio hilo. Hata hivyo wanasema watajitahidi".

"Kwa kutokana na hali ya namna hiyo serikali imeamua kutupa sisi jukumu hili, ingawa polisi wataendelea na upelelezi kamambe juu ya tukio hilo. Na ndio sababu nimeitwa kurudi mara moja toka likizo. Kwa hiyo toka sasa hivi ahirisha mambo yako mengine yote na tushughulikie tukio hili. Umenielewa?".

"Bila shaka".

Nilianza kumweleza jinsi nilivyoendesha mipango yangu yote nikiwatumia Sherriff na Veronika.

"Kwa hiyo Eddy, ninachotaka wewe ufanye, kwanza, nataka ukodishe magari manne kutoka kwenye kampuni mbali mbali zinazokodisha magari hapa mjini kama vile Co-cabs, Safari Toures Afrika Ltd., Takim's Agancies, nk. Gari moja kati hizi liegeshe mahali pa kuegesha magari New Afrika Hoteli na lingine liegeshe Kilimanjaro Hoteli. Magari mawili yatakayobaki nataka wewe pamoja na kijana mwingine kati yetu mtufuate kila mahali tutakapokwenda leo. Lakini mtufuate kwa siri kabisa kiasi kwamba mtu yeyote asitambue kama mnatufuata sisi. Mimi nitatumia gari langu. Nia yangu nataka muwe macho kama kuna watu wengine watakaoweza kuwa wanafuata safari yetu kwa siku ya leo. Umeelewa?".

"Nimeelewa vizuri kabisa bosi. Kazi itatekelezwa. Si ajabu hata wewe hutatuona."

"Kazi ya namna hiyo ndio nataka".

"Utapata, bosi."

"Gari zile utakazoziegesha New Afrika na Kilimanjaro Hoteli, weka swich ya gari hizi chini ya zuria kwa upande anaotoka dereva."

"Nitafanya hivyo."

"Haya sasa nenda ukashughulike na kazi hii ili saa nne muwe tayari nje ya New Afrika Hoteli ambapo ndipo tutaanza safari yetu."

"Tutakuwa hapo saa hizo, usiwe na wasiwasi".

ITAENDELEA



Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU