LOWASSA AWAAGA WANAFUNZI KIDATO CHA SITA BENJAMINI MKAPA

 Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akipokelewa na wanafunzi wa Kidato cha Sita, wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, alipofika leo kwa ajili ya kuwakabidhi vyeti vya kuhitimu na kuwaaga
Karibu Baba, ndivyo Lowassa alipokuwa akipokelewa na wanafunzi wa Benjamin Mkapa leo.
Lowassa akipunga mkono wakati akiwasili kwenye viwanja vya Shule hiyo kwa ajili ya kukabidhi vyeti na kuwaaga rasmi wahitimu wa kidato cha sita, Dar es Salaam leo
Hapa Lowassa anavutiwa na mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri mdogo zaidi kuliko wote.
Karibu Mheshimiwa, ndivyo alivyosema Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Bw. Maneno Mbegu (kushoto), wakati akimpokea Lowassa leo.
Hapa Bw. Mbegu (kushoto), akimtambulisha Lowassa kwa wazazi na wanafunzi walioshiriki mahafari ya kidato cha sita Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wakipiga makofi kumpokea mgeni rasmi, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa. 
Hapa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (katikati) na viongozi wa Shule hiyo wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa, wakati wa mahafari ya kidato cha sita leo.
 Wanafunzi wasanii wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa akifanya onyesho la igizo la mfano wa vijana wanaokosa elimu huishia kushiriki katika matukio ya uhalifu kaa wanavyoonesha katika mchezo wao leo.

Hapa Mzee akiagizwa avue viatu, huku akionyeshwa panga lenye makali.
Hawa ni baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika sanaa ya mitindo ya mavazi na umisi, wakati wa mahafari ya kidato cha sita leo.
 Wasanii wa Shule hawakusita kumshika mkono Waziri Mkuu Mstaafu baada ya kuvutiwa na uigizaji wao
 Hapa wakipiga picha ya pamoja kuonesha jinsi Lowassa anavyopenda sanaa.

 Mwanafunzi huyu ndiye aliyemgusa zaidi Lowassa baada ya kuigiza igizo la kuvutia lililouteka umma wa wananchi walioshiriki katika mahafari hayo
 Karibu uzungumze na wazazi na wanafunzi wa Benjamin Mkapa, Maneno Mbegu (kushoto), akimkaribisha Lowassa kuzungumza na wananchi leo.
 Hamjambo ndugu zangu, ndivyo Lowassa alivyoanza kuwasalimia wananchi.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru