MUUNGANO UKO SAWA, TUSIKWEPE KUJIBU MASWALI YA TUME YA WARIOBA


Tangu aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (pichani) akabidhi Rasimu ya Pili ya Katiba, kumekuwa na chokochoko, visa, matusi na  kejeli   kwa wajumbe wenzake hasa kwa sababu rasimu hiyo imependekeza muundo wa muungano wa Serikali tatu.
Rais Jakaya Kikwete alianza kukosoa muundo huo alipokuwa akifungua Bunge  Maalumu la Katiba akisema kuwa utazaa serikali legelege ya Muungano na itashindwa hata kulipa mishahara ya jeshi hivyo laweza kupindua nchi.
Baada ya hapo, basi ndiyo wajumbe wa CCM wamejawa mori na kuanza  kuvurumisha kejeli kwa Warioba na tume yake. Wengine kama Waziri William Lukuvi wamekwenda hadi kanisani na kuanza  kuwatisha  wananchi kuwa jeshi litapindua nchi kama Serikali zitakuja.Kituko zaidi ni maelezo ya mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba aliyesema kuwa ataingia msituni endapo serikali tatu zitakuja.
Ni kauli za aibu ambazo huwezi kutegemea kuwa zinaweza kutolewa na waheshimiwa wetu. Kama kauli hizo zingetolewa na wabunge wa upinzani basi ndiyo usiseme. Hivi haya malumbano yote ni ya nini ikiwa lengo ni kuboresha tu Muungano? Ingekuwa kweli kwamba Jaji Warioba ametangaza kuvunja muungano kweli,  wote tungemlaumu. Lakini kama lengo ni kuboresha, tatizo liko wapi?
Hivi karibuni, Jaji Warioba amehoji maswali saba ambayo kama yatapatiwa majibu na wanaopinga muundo wa Serikali tatu basi tuendelee na muundo uliopo. Nifafanua tu hapa machache. Kwanza, kwa nini wanapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi. Wiki iliyopita katika safu hii niliuliza, kama Rais Kikwete na wanaCCM hawakutaka muundo huu, kwa nini waliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilihali wakijua kabisa tume kama hizo zilishatoa mapendekeo kama hayo?
Kama wananchi ndiyo wanataka serikali tatu, kwa nini wapingwe? Kama wananchi wanapingwa basi tukubaliane kuwa muungano huu siyo wananchi bali ni viongozi na masilahi yao.
Jaji Warioba na baadhi ya wajumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba wakiteja jambo kabla ya kuwasilisha rasmu ya Katiba Mpya Bungeni Dodoma iliijadiliwe na wabungeComments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru