NDOTO ZA YANGA KUIFUNGA SIMBA

Wachezaji wa timu ya soka ya Yanga (pichani), wakishangilia moja ya magoli waliyofunga uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara. Mikakati ya Yanga kuwafunga wapinzani wao wa jadi katika soka la Tanzania Bara Simba ni sawa na ndoto ya mchana, kutokana na viongozi wa timu hiyo ya Jangwani, Jijini Dar es Salaam kung'ang'ania kusajili wachezaji wa Klabu hiyo ya Msimbazi.

Yanga Klabu Bora kabisa katika Ligi Kuu ya Tanzania, kutokana na kuwa na wachezaji wengi wenye vipaji vya hali ya juu, wameshindwa kabisa kuwafunga watani wao Simba, ambao msimu uliopita walikuwa na kikosi dhaifu ambacho kimeambulia nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom mwaka huu.

Yanga timu pekee iliyofunga mabao mengi kwenye ligi kuu ya Vodacom, ikiwa pamoja na kufunga mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Mlandizi, pia ikawashushia kipigo kitakatifu wababe walioifunga Simba 3-2 Uwanja wa Taifa JKT Ruvu kwa mabao 5-0, lakini wakashindwa kutamba mbele ya Simba walipokutana mara mbili na kuambulia sare.

Katika mchezo wa kwanza, Yanga iliyokuwa mbele kwa mabao 3-0, huku mashabiki wake wakiamini kuwa wachezaji wao wanarejesha heshima na kulipa kisasa cha mabao 5-0 waliyofungwa na Simba mwaka juzi. Tofauti na matarajio ya wengi, Simba walirudi uwanjani na molali mkubwa na kufanikiwa kurejesha mabao hayo huku mashabiki wa Yanga wakizimia majukwaani.

Katika mchezo wa pili ambao baadhi ya mashabiki wa Simba waliofika uwanjani hawakuwa na matumaini na kikosi chao, kutokana na kupoteza mwelekeo wa kupata nafasi tatu za juu, Simba waliwashangaza mashabiki kwe kucheza kandanda safi na kutangulia kupata bao la kuongoza na kuwafanya Yanga kuhaha kutafuta bao la kusawazisha lililofungwa na Simon Msuva.

Kutokana na tathimni hiyo, Yanga wanapaswa kujitafakari, kuna nini ndani yao, wakati umefika Yanga waache kusajili wachezaji kutoka Simba kwani wanaongeza mamuluki ndani ya kikosi chao hata kiwe kizuri kiasi gani. Wajiulize kwanini Simba walirejesha mabao 3-0 waliyofungwa kipindi cha kwanza. Kwanini Simba walipata ushindi wa 3-1 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe na Simba waliwezaje kuwafunika wachezaji wa Yanga wenye uwezo wa kuzishinda timu zingine zaidi ya mabao 5.
Furaha ya Ushindi, Wachezaji wa Yanga, Nadir Kanavoro (kulia), Simon Msuva (katikati) na Joshua wakishangilia baada ya kupata bao

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU