TANZANIA YAILAZA ZIMBABWE, MASHABIKI WASHANGAA MABADILIKO YA KOCHA NOOIJ


KIKOSI KAMILI CHA TIMU YA SOKA YA TANZANIA 'TAIFA STARS', KILICHOCHEZA NA ZIMBAWE NA KUPATA USHINDI MWEMBAMBA WA BAO 1-0 UWANJA WA TAIFA.


KIKOSI KAMILI CHA TIMU YA TAIFA YA ZIMBABWE KILICHOFUNGWA BAO 1-0.

Na Nyakasagani Masenza, Dar es Salaam
UDHAIFU na kutojiamini kwa Kocha Mkuu mpya wa timu ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars Mart Nooij, raia wa Holland umewafanya watanzania kukosa ushindi mnono dhidi ya timu ya Tafa ya Zimbabwe, zilipokutana kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam kusaka tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, nchini Morocco.

Udhaifu huo wa Kocha umeifanya Tanzania kuambulia bao moja dhidi ya Zimbabwe ambao wameonekana kufurahia matokeo hayo, japokuwa Tanzania ilikuwa na uwezo wa kupata mabao mengi zaidi katika mchezo. Kiungo wa mshambuliaji wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto pamoja na kuonyesha udhaifu katika safu ya ushambuliaji, Kocha Noolj alimwacha aendee kufanya madudu uwanjani.

Tanzania iliyohitaji ushindi mnono katika mchezo huo muhimu, iliambulia bao hilo lililofungwa katika dakita ya 23, kipindi cha kwanza na mshambuliaji mwenye nguvu, John Boko, akiunganisha mpira uliopigwa kwake na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu, anayekipiga katika Klabu ya T.P Mazembe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kuingia kwa bao hilo pekee katika mchezo huo, liliamsha shangwe na ndelemo kwa mashabiki wa Tanzania waliofika uwanjani, wakisubiri kupata mabao mengine zaidi ili kusherehekea ushindi mnono utakaoisaidia Tanzania katika mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Zimbabwe, lakini mambo hayakuwa hivyo kutokana na mabadiliko ya wachezaji yaliyofanywa na Kocha.

Mashabiki wa Tanzania walishangazwa na kitendo cha Kocha Noolj kuwmtoa kiungo mkabaji Frank Domayo, aliyesimama vizuri katika nafasi yake na kumwingiza Amri Kiemba, ambaye alipaswa kuingi badala ya Mwinyi Kazimoto ambaye uchezaji wake haukuendana na washambuliaji wa Stars, Mbwana Samata, Mrisho Ngassa, Ulimwengu na Boko, waliokuwa wakishirikiana vizuri.

Kocha Nooij pia alifanya makosa makubwa kuwatoa washambuliaji Ngassa na Boko, waliokuwa wakihaha uwanjani na kuwatia hofu wapinzani wao na nafasi zao kuchukuliwa na Haruna Chanongo na Khamis Mcha. Kuingia kwa wachezaji hawa kuwaliwafanya Wazimbabwe kate mstari na kuhamia kwenye goli ya Tanzania.

Aina hii ya uchezaji kwa timu ya Taifa, bado ni safari ndefu kwa watanzania kuelekea kwenye fainali za kombe la Dunia 2018 na Mataifa ya Afrika nchini Morocco. Katika safu ya ulinzi, Nahodha Nadir Haroub 'Kanavaro', Kelvin Yondani na Oscar Joshua walicheza kwa ushirikiano, japokuwa Shomali Kapombe alifanya makosa madogo ambayo aliyerekebisha.

Zimbabwe ni moja ya timu nzuri yenye wachezaji wengi wanaoujua mpira kama Nahodha wao Partson Jaure, Danny Phiri na biki wa mwisho Stephen Alimenda. Zimbabwe inao washambuliaji wenye kasi kama Eric Chipeta, Peter Moyo, Cuthbert Malajila na kiungo mshambuliaji Kadakwashe Mahachi.

Iwapo Tanzania inahitaji kushinda mchezo wa marudiano na kusonga mbele, inapaswa kufanya mambo matatu, kuimalisha sehemu ya ulinzi, kiungo mshambuliaji, Amri Kiemba na Jonas Mkude wanazo sifa ya kusimama katika nafasi hii. safu ya ushambuliaji Simon Msuva asiachwe benchi.

KOCHA WA TIMU YA TANZANIA  MART NOOIJ NA BENCHI ZIMA LA TIMU HIYO


WACHEZAJI WA STARS WAKIWAPUNGIA MASHABIKI IKIWA NI ISHARA YA USHINDI DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA ZIMBABWE, UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM.

"EWE MWENYEZI MUNGU TUSAIDIE TUPATE USHINDI DHIDI YA ZIMBABWE", NDIVYO WACHEZAJI WA STARS WANAVYOOMBA DUA KABLA YA MCHEZO NA KUSHINDA  1-0.



Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU