NSSF YAMSAIDIA MLEMAVU WA VIUNGO KUPATA BAISKELIAfisa Utawala wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Temeke, Bw. Rashid Msaka (kulia), akisalimiana na mlemavu wa viungo Bi. Mariam Mtoro, mjini Kibaha, baada ya kumpatia msada wa Baiskeli iliyotolewa na shirika hilo kwa ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii. Kushoto Afisa Mafao wa Temeke,Bw. Adili Gurumo, Bw. Iddy Mpole na Baba mzazi wa Mariam, Bw. Peter Nhosha wa pili kulia.
 Bi. Mariam akiwa ameketi kwenye Baiskeli yake baada ya kukabidhiwa na maofisa wa NSSF
 Kama maandishi yanavyosomeka 'DONATED BY NSSF', imetolewa kwa msaada wa NSSF
Afisa Mafao wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoa wa Temeke, Bw. Adili Gurumo (kushoto), akikabidhi mssada wa Baiskeli iliyotolewa na shirika hilo kwa mlemavu wa viungo, Bi. Mariam Mtoro, mjini Kibaha juzi, ikiwa ni mpango wa kusaidia jamii. Kulia ni Afisa Utawala wa NSSF Temeke, Bw. Rashid Msaka na Dereva Bw. Iddy Mpole.
 Hapa maofisa wa NSSF wakifurahia jambo pamoja na Mariam nyumbani kwao Kibaha,mkoani Pwani
Hapa wakiangalia jinsi Mariam anavyoweza kutumia Baiskeli hiyo kwa shughuli zake binafsi.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru