WATANZANIA WANAHITAJI RAIS MWENYE SIFA ZA LOWASA

Waziri Mkuu Aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowasa (pichani), ndiye kiongozi anatajwa na idadi kubwa ya Watanzania kuwa kiongozi makini wenye kipaji cha uongozi na sifa zinazofaa kurithi mikoba ya Rais Jakaya Kikwete, anayemaliza muda wake wa uongozi mwaka 2015, lakini Lowasa akikabiliwa na changamoto nyingi kutoka kwa mahasimu wake kisiasa.

Wakati huu ambapo Watanzania wanasubiri Bunge la Katiba lipitie Rasmu ya Katiba Mpya, baadhi ya wanasiasa wameanza kuunda makundi kwa ajili ya kuwachafua viongozi wenzao hususan wanaowaona kuwa ni tishio kwao, jambo ambalo likiachwa liendelee linaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa kwa jamii.

Edward Lowasa anatajwa kuvaa viatu vya Mtangulizi wake, Hayati Edward Moringe Sokoine kutokana na msimamo tunayemkumbuka kila Aprili 12. Kitendo cha kuwatetea vijana husasan aliowawezesha kusoma katika shule za Kata alizoziasisi yeye alipokuwa Waziri Mkuu, zimesababisha vijana wengi wa vijijini kupata elimu ya Sekondari. Huku wakisema kama Lowasa angeendelea kuwa Waziri Mkuu shule hizo zingekuwa na kiwango bora zaidi cha elimu.

Utendaji kazi wa Lowasa wakati akiwa Waziri Mkuu ulivuta hisia za wengi, baada ya kuwawajibisha baadhi ya watendaji walioshindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa ngazi za juu walishindwa kuchukua maamuzi kama hayo wakihofia nyadhifa zao. Lowasa alithubutu akaweza

Wakati huo katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015, yameibuka makundi ndani na nje ya vyama vya siasa kwa ajili ya kupakana matope, jambo ambalo kwa kiasi fulani halifai kuwepo katika siasa za Tanzania, taifa lenye sifa ya amani na utulivu. Kutokana na sifa hizo Watanzania wanahitaji kiongozi wa mfano na msimamo usioyumbishwa kama Lowasa.

Akiwa katika wadhifa wa Waziri Mkuu, Lowasa alifanya kazi kubwa ya kupita kwenye Halmashauri zote nchini kuangalia utendaji kazi wa Halmashauri hizo, huku akichukua maamuzi magumu ya kuwatimua kazi watendaji walioshindwa kutumiza majuku yao na kusababisha wananchi kupata usumbufu.

Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowasa akizungumza na waandishi wa habari katika moja ya mikutano yake ya kisiasa. WATANZANIA WANAHITAJI RAIS MWENYE SIFA ZA LOWASA ILI TAIFA LIWEZE KUSONGA MBELE, KUTOKA HAPA TULIPO.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru