Kocha wa Yanga, Marcio Maximo
KATIKA hali
isiyokuwa ya kawaida, siku chache baada ya mchezo wa mahasimu wa Soka la
Tanzania, Yanga na Simba, mashabiki wa Klabu ya Yanga wamemwaga shutuma nzito
kwa Kocha wao Marcio Maximo, kuwa alichangia kwa kiasi kikubwa timu yao kutoa
sare ya bila kufungana na Simba.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wakati mchezo ukiendelea na baada ya mchezo huo, Yanga
wenye kikosi bora kuliko wapinzani wao Simba, walitegemea kupta matokeo mazuri,
lakini badala yake timu hizo zikatoka sare tasa.
Salmu Rupia
kutoka Zanzibar, alikuwa wa kwanza kulaani matokeo hayo, akisema yamechagizwa
na ubishi wa Kocha wao Maximo, aliyewachezesha wachezaji anaowataka yeye,
Santana Jaja na Andre Continho, ambao walionyesha kiwango kidogo tofauti na
wenzao Simba.
Samwel
Kitundu wa Yombo yeye alisema, Simba wana kila sababu ya kushangilia matokeo ya
sare, kwani mashabiki wao hawakuwa na matumaini ya kushinda, lakini wakaonyesha
kiwango kizuri, kutokana na sehemu ya kiungo ya Yanga kuzidiwa kwa sababu
wachezaji hao hawakuwa na msaada.
“Maximo
alipaswa kuwaanzisha wachezaji wenye kasi kama Jerrison Tegete anayewajuwa
Simba ndani nje na winga mwenye kasi ya ajabu Simon Msuva, ambaye aliingia
dakika 20 za mwosho”, alisema Kitundu na kuongeza kuwa lawama zmuendee Maximo
kwa ubishi wake.
Comments
Post a Comment