KATIKA moja ya Makala zangu kupitia MPIGANAJI, niliwahi kuandika kuwa Kocha wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo, ameisaidia Simba kupata sare dhidi ya Yanga, kwa kulazimisha kuwachezesha wabrazil wenzake, Santos Jaja na Andy Continho.
Ukweli huo
ulidhihirika Jumamosi iliyopipa, Ynga ilipocheza na Stand United ya Shinyanga, na
kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0, mawili yakifungwa na mshambuliaji nguli
wa Yanga, Jerrison Tegete, aliyeingia kabla ya dakika 19, akichukua nafasi ya
Jaja.
Hakuna
ubishi kuwa Maximo ni Kocha mzuri, lakini kulazimisha kuwatumia wachezaji hao
kila mchezo kunaifanya timu kuzidiwa kutokana na aina ya uchezaji wao kwani
hawakabi adui, isipokuwa wanasubiri kuletewa mipira ili wafunge.
Wakati umefika kama Kocha Maximo anataka kuwafurahisha wapenzi na mashabiki wa Yanga, awatumie Tegete, Hussen Javu na Nizar Khalfan, ambao kutokana na umakini wao uwanjani, wanaweza kuisaidia timu kushinda mchezo wowote.
Tegete ni
aina ya mshambuliaji anayetakiwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Yanga, kwani
msimu uliopita pamoja na kucheza mechi sita tu, tena akitokea benchi, aliweza
kufunga mabao 6, tofauti na wenzake Didie Kavumbangu aliyehamia Azam, alifunga
mabao 7 pamoja na kucheza mechi karibu zote 23.
Kwa mahesabu
ya haraka, kama Kocha Maximo ataacha upendeleo kwa Jaja na Continho, awatumie
japo kipindi cha akina Tegete, Nizar Khalfan na Hussen Javu, watawafunika
kabisa wabrazil hao.
Comments
Post a Comment