Na Nyakasagani Masenza
UNAWEZA kusema nani
jeuri leo, unapozungumzia mchezo wa leo kati ya mahasimu makubwa wa soka la Tanzania Yanga na Simba, zenye
mashabiki wengi, lawama kwa makocha na waamuzi husika, Zinashuka dimbani Taifa leo kila mmoja akikamia kushinda mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mchezo huu unasimamiwa
kwa sheria kumi na saba za soka, ambazo pamoja na waamuzi wengi kuzisimamia kwa
umakini mkubwa zaidi, lakini minung’uniko hutawala hususan kwa timu
zinazopoteza mchezo.
Tanzania kama
yalivyo Mataifa mengine duniani, inazo timu za soka zinazoshiriki ligi za
madaraja mbalimbali, kuanzia Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na ile ya Zanzibar hadi
ligi za madaraja ya chini.
Oktoba 18 leo Alasiri,
mahasimu wakubwa wa soka la Tanzania, Yanga Afrika kutoka Jangwani, wakiwa
chini ya Mwalimu mhamasishaji Mbrazil Marcio Maximo, watashuka uwanja wa Taifa Dar
es Salaam kuonyeshana umwamba na Simba Sport Klabu ya Msimbazi, chini ya
kocha mwenye rekodi nzuri, Mzambia Patrick Phiri kuwania pointi tatu muhimu za
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ni vigumu kutabiri
mshindi wa mchezo huo, ambao kwa mara ya kwanza utawakutanisha wachezaji wawili
waliozusha gumzo kubwa katika usajili, Mbrazil Santos Santana Jaja na Mganda
Emanuel Okwi, ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitamba kuonyesha maajabu
kuwa watazifungia timu zao mabao muhimu.
Yanga ndio wenye kikosi
bora msimu huu, ikiwa imesheheni wachezaji wenye uwezo mkubwa, kama Nahodha
Nadir Haroub ‘Canavaro’, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mrisho Khalfan Ngassa,
Mbuyu Twite, Jaja na Hassan Dilunga, Continho na Simon Msuva.
Simba pia inaundwa na
kikosi cha wachezaji wenye uwezo na kasi ya kushindana kama Emmanuel Okwi, Amis
Tambwe, Ramadhan Singano, Jonas Mkude, Shaaban Kisiga, Joseph Owino na Amri Kiemba.
Japokuwa timu hiyo imekuwa haifanyi vizuri msimu huu kwa matokeo ya sare
mfululizo, inaweza kufanya maajabu pia.
Ni vigumu kutabiri
matokeo ya mchezo wa leo kutokana na rekodi za timu hizo, Yanga ilikuwa na
rekodi nzuri wakati wa Abbas Guramali na Mohamed Vilan Babu, wote marehemu,
wakiifunga Simba watakavyo, hatmaye mambo yakabadilika Simba nao wakaanza
kulipa kisasi.
Simba wanaweza kuwa na
nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa leo kutokana na hali halisi ya mchezo. Ni
rahisi Simba kuwatumia wachezaji wao wa zamani walioko Yanga kupata ushindi,
japokuwa ni vigumu kuamini hilo. Ndani ya Yanga kuna wachezaji
waliosajiliwa kutoka Simba, Juma Kaseja na Kelvin Yondani.
Kama nilivyowahi
kusema siku za nyuma, mchezo wa Yanga na Simba huchezwa kwa mbinu za hapa na
pale, lakini Yanga ndio waathirika wakubwa, kwani hucheza uwanjani wakiwa
pungufu, huku wenzao Simba wakiwa zaidi. Wakisaidiwa na wenzao ndani ya Yanga.
Kimtazamo Simba hawana
ubavu wa kushindana na Yanga, baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiangalia matokeo
ya awali ya timu hizo, ambapo Yanga wameshinda mara mbili dhidi ya Prison ya
Mbeya na JKT Ruvu na kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa mkoani Morogoro.
Simba hajapoteza mchezo,
lakini imepata sare tatu Uwanja wa Taifa Dar es Saslaam, wakianza kupata mabao
ambayo hayadumu dhidi ya Coastal Union ya Tanga 2-2, Polisi Morogoro 1-1 na
Stand United ya Shinyanga 1-1. Matokeo ambayo yanaongeza hofu na ushindani
katika mchezo wa leo.
Macho na masikio ya
mashabiki wa soko yanaelekezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo,
huku tegemeo la timu hizo ni washambuliaji wawili tegemeo, Jaja kwa upande wa
Yanga na Okwi Simba.
Katika mchezo wa mwisho
kwa timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1, Simba wakitangulia kupata
bao lililofungwa na ….. Yanga walisawazisha kupitia kwa Simon Msuva.
KIUNGO MSHAMBULIAJI TEGEMEO LA YANGA HARUNA NIYONZIMA
KIKOSI CHA SIMBA KINACHOSHUKA DIMBANI LEO KUONYESHANA KAZI NA YANGA
MSHAMBULIAJI MSUMBUFU WA SIMBA EMMANUEL OKWI, ALIYETAMBA KUIFUNGA YANGA LEO
JAJA WA YANGA AKIONYESHA VITU VYAKE UWANJANI
AMISI TAMBWA WA SIMBA
MAKOCHA WA YANGA
MAKOCHA WA SIMBA
Comments
Post a Comment