MELI YA UJERUMANI YATIA NANGA DAR, WANAJESHI WAPONGEZWA

Baadhi ya Maofisa na wanajeshi wa Jeshi la Ujerumani, wakiwa mbele ya eli ya kivita ya nchi hiyo FGS Lübeck wakati hafla ya kukipongeza kikosi cha wanamaji wa Ujerumani kilichoongozwa na Kamanda Peter Christian Semrau.
Balozi wa Ujerumani nchini Egon Kochanke (kushoto) akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania wakati wa hafla ya kuwakaribisha na kuwapongeza wanajeshi wa kikosi cha wanamaji wanaotumia meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck kufanya doria ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya Jeshi la Kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta chini ya Kamanda Peter Christian Semrau (kulia) Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
 Maofisa wa Jeshi, Mabalozi, wageni na wanajeshi wakipata kinywaji ndani ya Meli ya Kivita Dar es Salaam
Balozi wa Ujerumani nchini Egon Kochanke (kushoto) akigonganisha glasi na Kamanda Peter Christian Semrau wa kikosi cha Jeshi la Maji la Ujerumani huku wanajeshi wengine wakishuhudia, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanajeshi wa kikosi hicho, Jijini Dar es Salaam
 Askari wa Jeshi la Ujerimani wakijipongeza kwa kinywaji baada ya kutia nanga Jijini Dar es Salaam, ambapo walifanyiwa sherehe maalumu ya kupongezwa kutokana na jitihada zao za kulinda amani Baharini
Wanajeshi wa Jeshi la Maji la Ujerumani wakionyesha utimamu wa mwili ndani ya Meli ya Kivita ya Ujerumani iliyotia nanga Dar es Salaam. Meli hiyo ni maalumu kwa ajili ya doria za Baharini kwa ajili ya uhalifu wa kivita
 Baadhi ya Makamanda ndani ya Meli hiyo wakiteja jambo wakati wakiendelea na kinywaji, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akihoji jambo kwa mmoja wa askari wa kikosi cha maji kwenye Meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru