GISENYI
IX
Meja
Kasubuga baada ya kuachana na Willy Gamba, alimtafuta Col. Rwivanga akitumia
simu ya Satellite na kumweleza kuwa Willy alikuwa amefika salama na kwamba Willy na Bibiane walipanga kuelekea Kibumba usiku uleule.
Col.
Rwivanga alifurahi kupata simu ya Meja Kasubuga lakini akakataa Willy na mwenzake wasiondoke, "Hapana mwambie Willy na
mwenzake wasiondoke mpaka kesho, kuna mabadiliko ya mipango ya kazi huku, waambie
wapumzike tu hakuna tatizo. Meja Tom Kabalisa atakuja kumuona Willy kesho asubuhi, nami nitafika
huko kesho asubuhi. Hivyo, mambo yote tutapanga kesho baada ya sisi kufika
huko".
"Nimekusoma,
nitamweleza kuhusu taarifa hii afande".
Kasubuga
aliona si vyema kumweleza Willy wakati ule, bali amwache mpaka baadaye ili
apumzike kidogo, lakini muda si mrefu alikuja askari mmoja na kusema kuwa wale
wageni wa Msalaba Mwekundu walikuwa wakihitaji chakula. Meja Kasubuka akaona
huo ulikuwa muda mwafaka vilevile kuwaeleza kuhusu maagizo kutoka kwa Col.
Rwivanga. Hivyo, akaamua yeye mwenyewe ndiye awapelekee chakula kitakapokuwa
tayari ili awaeleza kama alivyoagizwa.
"Chakula
kilipokuwa tayari Meja Kasubuga aliwapelekea yeye mwenyewe na kuwaeleza kuhusu maagizo aliyopewa kutoka
kwa Col. Rwivanga.
"Sawa
tumekusikia", Willy alijibu bila kuonyesha kama alikuwa na maana gani au alipanga kufanya nini usiku ule.
ITAENDELEA
0784296253
Comments
Post a Comment