MICHUANO YA NSSF MEDIA CUP 2015 YAFIKIA PATAMU

TIMU YA SOKA YA WAANDISHI WA HABARI WA MWANANCHI COMMUNICATION WALIOTINGA HATUA YA PILI BAADA YA KUWAFUNGA RADIO MARIA TCC KWA MIKWAJU YA PENATI 4-2 KWENYE VIWANJA VYA TCC CHANG'OMBE.
 ............................................................................................................................................


Na Mwandishi Wetu
Mashindano ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa Vyombo vya habari ya ‘NSSF Media Cup 2015’ yameendelea kuonyesha msisimko na ushindani wa aina yake baada ya timu vigogo kupata ushindi na zingine kuondolewa katika michezo ya awali.

Mashindano hayo yanafanyika wakati wa wiki ya Huduma Kwa wateja wa NSSF ambao watapata fursa ya kupata elimu kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo, ambapo wanachana watapata taarifa za michango yao na wengine wataandikishwa uanachama wa hiari.

Mashindano hayo yanayoendeshwa kwa mtindo wa mtoano, yalianza Machi 14, mwaka huu  baada ya kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa ufunguzi, TBC ilifanikiwa kuitupa nje Free Media kwa bao 1-0 lililofungwa na Ahamed Salim, nao IPP wakaifungasha virago TSN kwa bao 1-0 lililofungwa na Urio, huku Mwananchi Communition wakatinga hatua ya pili kwa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya Radio Maria, baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa bao 1-1.

Katika mchezo mwingine uliochezwa kwenye viwanja vya TCC, timu ya Azam Tv iliyokuwa chini ya Kocha wao mwamuzi mkongwe Othman Kazi walikubali kipigo kitakatifu cha mabao 5-0 kutoka kwa Clouds Media.

Kwenye viwanja vya Bandari, New Habari walifanikiwa kuwafungisha virago wakongwe wa michuano hiyo, Business Times kwa mikwaju ya penaali, nao Habari Zanzibar wakafanikiwa kuwashinda Radio Heri 3-0.

Hadi tunakwenda mitamboni timu za NSSF na Jambo Leo zilikuwa zikichuana vikali kwenye viwanja vya TCC kuwania nafasi ya kusonga mbele, wakati Uhuru Communication nao wakionyesha umwamba na Sahara Media.

Kupitia mashindano hayo, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Salim Kimaro amewataka wanachama wa shirika hilo waishio Dar es Salaam kufika kwa wingi kwenye viwanja vya TCC kujua maendeleo mafao yao.


NAHODHA NA MSHAMBULIAJI WA MWANANCHI COMMUNICATION JULIUS KIHAMPA (KULIA) AKIUTAMANI MPIRA ULIODAKWA NA KIPA WA RADIO MARIA, YONA MNG'ONG'O 
MLINZI WA RADIO MARIA FRED WANGAO (KUSHOTO) AKIMLINDA JULIUS KIHAMPA WA MWANANCHI ILI ASIMFIKIE KIPA WAKE. MWANANCHI WALISHINDA KWA PENATI 4-2.
JULIUS KIHAMPA WA MWANANCHI COMMUNICATION AKITAFUTA MBINU ZA KUMTOKA MLINZI WA RADIO MARIA FRED WANGAO, TI,U HIZO ZILIPOCHUANA JANA.
MLINZI KISIKI WA MWANANCHI COMMUNICATION, SALUM JABA (KULIA), AKIMCHUNGA VILIVYO MSHAMBULIAJI WA RADIO MARIA MUSSA JUMA.
WACHEZAJI WA RADIO MARIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MWAMUZI WA MCHEZO HUO PAMOJA NA NAHODHA WA MWANANCHI MAJUTO OMARI BAADA YA WACHAZAJI WA TIMU HIYO KUTILIWA SHAKA KUWA SI WAANDISHI WA HABARI
MLINZI WA MWANANCHI HATIMU NAHEKA (KUSHOTO) AKIJARIBU KUWAHI MPIRA MBELE YA MSHAMBULIAJI HAMIS NGUMBE WA RADIO MARIA.
KATIBU MKUU WA ZAMANI WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF), ANGETILE OSIAH (KULIA) AKIUCHEZEA MPIRA HUKU GERALD MOSES WA RADIO MARIA AKIWA MAKINI
ANGETILE AKITAFUTA MBINU ZA KUMTOKA GERALD MOSES WA

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU