UCHU

KASHESHE

XVII

Col. Rwivanga, Mpinda na Meja Tom Kabalisa waliwasili mpakani mwa nchi za Rwanda na Zaire katika sehemu waliyokuwa wamekubaliana na Meja Kasubuga mnamo saa nane na dakika arobaini usiku.

Hali ya usalama ilikuwa imeimalishwa katika eneo hili, ambapo vijana wa Meja Kasubuga walikuwa makini kwa kila jambo, baada ya Helikopta ya jeshi la Rwanda waliyosafiri hadi mpakani kutua, Col. Rwivanga alikuwa wa kwanza kushuka akifuatiwa na Mpinda, kasha Meja Kabalisa.

"Mambo yakoje hapa", Col. Rwivanga alimuuliza Meja kasubuga wakati wakisalimiana baada ya heshima ya kijeshi.

Meja Kasubuga alieleza kwa urefu jinsi mapambano yalivyokuwa, kisha akamalizia, "Huyu Willy atakuwa kauawa kule Kibumba maana kajipeleka mahali ambapo panatakiwa vikosi vyote husika, huyu Willy ingawaje Afande unamsema ni hatari lakini hana akili ya tahadhari, angesubiri twende wote, ndipo angeweza kuwa msaada kwetu maana maiti haina msaada wowote.

"Nakubaliana na wewe lakini yule ni mtu mwenye maisha mengi, unaweza kumuona kaibuka", Col. Rwinga alisema wote wakacheka kwa utani huo.

"Kweli, akiibuka tena atakuwa mtu wa maisha mengi", Meja Tom Kabalisa wa Banyamulenge alijibu kwani na yeye alijua nguvu za Intarahamwe kule Kibumba na ndio sababu alikuwa hajathubutu kufanya lolote. Kisha akaendelea. "Col. Rwivanga, nafikiri sasa tumweleze Meja Kasubuga mipango ikoje ili....", Kabla Meja Kabalisa hajamaliza kusema sentesi yake, mripuko mkubwa usio kifani ulisikika mpaka huko walikokuwa.

"Ooh Willy Gamba, kweli u-hatari", Meja Kasubuga aligwaya.


ITAENDELEA 0784296253

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru