SURA YA SABA
Proper alikuwa ameketi katika chumba chake cha kusomea aliposikia kengere ya mlango ikilia akashituka. Akainua kichwa kwa mshangao. Hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kugongewa mlango akiwa chumbani. Majirani zake walifanya ujirani wao wote nje. Rafiki zake 'bandia' aliwakaribisha nje kabisa ya nyumba hii.
Muda mfupi kabla ya mlango kugongwa, alikuwa akimalizia kuandika mpango wake kabambe ili baadaye auhariri, na kisha kuuingiza katika mtandao maalumu ambao ungeyrsafirisha maandishi hayo hadi mahali fulani katika nchi fulani huko Ulaya, kwa wakubwa zake. Mpango huo alikuwa ameubuni yeye binafsi, akauhakiki na kuona kuwa lazima utafanikiwa. Yangekuwa mafanikio makubwa ambayo yangeitetemisha Afrika na kuitikisa dunia nzima.
Kwa kuwa hili litakuwa pigo la aina yake, ambalo halijapata kuitokea dunia kwa muda mrefu. Pigo zito kama lile lililotokea wakati wa gharika lililoua watu wote na kumwacha Mungu na familia yake tu. Au kama lile bomu la Atomic lililopigwa na Mwamerika ambalo liliua maelfu ya Wajapani kule Hiloshima. Hili lake pia ingawa alikusudia kuziteketeza baadhi ya nchi, lakini litafanya machozi mengi yamwagike kiasi cha kufanya lisifutike katika kurasa za matukio ya kihistoria duniani.
Mafanikio lazima. Hakukiona kipingamizi chochote. Polisi walikuwa gizani wakitetemeka na kusubiri kwa hofu bila kufahamu wanachosubiri. Watakapotanabai, kazi itakuwa imekamilika. joram Kiango, ambaye alihofiwa kama tishio, ingawa yeye proper hakuona vipi angeweza kumletea vipingamizi, sasa yuko kuzimu. Wafu wenzake watamsimulia ilivyotokea.
Pengine tatizo lingetokana na viongozi wake huko Ugaibuni. Labda ni wao wangeweza kumpinga kutokana na woga wao. Lakini mpango huo ulikuwa wake binafisi, ameubuni, ameuandaa na lazima autekeleze. Imekwisha mgharimu muda na pesa nyingi, zake binafsi wakati akiuhakiki. Yeyote asingeweza kumshawishi abadili mpango wake, zaidi ya hayo, hakumbuki lini waliwahi kupewa changamoto nzito kama hiyo. Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Zaire (Congo), Patrice Lumbumba? Kuuawa kwa Rais Nguabi? Unyama aliofanyiwa Edward Mondolane wa Msumbiji? Hapana. Yeye Proper atafanya zaidi ya hayo. Ataifanya dunia ielekeze macho na masikio hapa.
Kengere ya mlango iliita tena. Ni nani huyo? Proper alijiuliza akificha vifaa vyake vyote. Haraka na kwa utaalamu aliuvua uso wa Proper na kujivika ule wa Profesa Chain Kimara wenye dalili zote za hekima na mshughuriko, uso uliomlaki Neema Iddy aliyekuwa amesimama mlangoni akijiandaa kubonyeza kengere kwa mara ya tatu.
"Karibu mama", Proper alisema huku akisimama kando kumpisha mgeni wake apite. Kichwani alikuwa kajawa na mshangao mkubwa. Sura nzuri ya msichana huyu haikuwa ngeni machoni mwake ingawa hakuwahi kuiona sura hii ana kwa ana kwa leo. Ilikuwemo katika majarada yake. Ilikuwa sura ya Neema, Katibu Mahsusi wa Joram Kiango. Amewezaje kunishuku mapema kiasi hiki? Proper alikuwa akijiuliza. Si kitu, alijiambia. Nilikosea sana kumsahau. Alistahili kufa kitambo. Alistahili kwenda na Joram. Madaamu kajileta mwenyewe.
"Dada, karibu ndani", Proper alimhimiza Neema.
"Asante, lakini sikai. Nilitaka... Ni..." Neema alikwama kidogo. Uso uliokuwa mbele yake hakuona kama ulifaa kusumbuliwa kwa maswali yaliyoeleweka. Aliuona kama uso wa msomi mwenye hekima na mengi, ingawa macho yake yalikuwa na kitu zaidi ya uso, alijiona mpumbavu kuja hapa bila subura. Huyu haelekei kuhusika katika kifo cha joram.
"Haraka ya nini?" Proper alimkatiza huku akimtengenezea tabasamu ambalo lilimtoa hofu Neema. "Utaingia ndani, utakaa, unywe walau chupa moja ya bia kisha tutaongea".
"Hapana, hapana", Neema alimkanusha, "Sitaki kuupoteza bure muda wako. Nilitaka ku..."
Alikatizwa tena, akashikwa mkono na kuvutwa ndani kistaarabu. Akaonyeshwa kiti ambacho aliketishwa polepole.
"Sikai sana. Samahani kwa kukupotezea muda wako, Nilitaka kujua kama unajua chochote kuhusu Joram Kiango?", alifaulu kuuliza.
"Joram! Namjua sana. Sidhani kama yupo mtu asiyemjua, Kifo chake kimenishtua sana. Alikuwa kijana wa ajabu sana". Kisha Proper alijitia kushituka kidogo alipouliza, "Unadhani ni kweli Joram Kiango kafa hivi hivi tu? Mimi siamini. Nadhani wamempa sumu. Wewe waonaje?" Neema alipochelewa kujibu, Proper alijitia kushituka tena, "Lakini wewe ni nani? Na ulitaka mimi niseme nini kuhusu Joram au unataka mawazo gani kutoka kwangu?".
Neema alijiona mjinga zaidi. Huyu msomi wa watu alionekana hajui lolote. Yawezekana yule mwanamke wa ajabu, Unono, alikuwa punguani pia. Picha ya mzee huyu pengine aliiokota au kuiiba mahala na kuileta kwake. Mzee huyu hakuonekana kujua chochote cha muhimu juu ya kifo cha Joram.
Haraka Neema akainuka na kuaga.
|Haraka hii? Proper alihoji kwa mshangao. Safari hii alionyesha mshagao halisi. Alikuwa akitafuta nafasi nzuri ya kumtia Neema mikononi mwake. Japokuwa kiti alichokalia Neema kingeweza kutimiza wajibu wake lakini Proper hakukusudia kutumia njia hii. Na njia hii ilikuwa rahisi zaidi. Proper angeweza kukanyaga mahala fulani chini ya meza kisha voti kadhaa za umeme zingepita katika kiti hicho na kumwua Neema papo hapo. Hakufanya hivyo kwa sababu mbili. Mosi, alikuwa bado hajafahamu msichana huyu anajua nini na anataka nini kwake, na pia hakutaka Neema afie nyumbani kwake.
"Huwezi kuondoka bila kunywa chochote? Siwezi kuruhusu binti mzuri kama wewe atoke nyumbani kwangu pasi ya kuonja chochote, Vilevile hatujazungumza".
"Samahani. Sijisikii kunywa chochote".
"Na uichotaka kuuliza juu ya Joram?".
"Nimebadili mawazo".
"Kwanini?".
Huku akianza kutoka ndani ya nyumba hii Neema alisema, "Nilikosea...".
Hakujua kilichompiga. Hakusikia maumivu yoyote. Alijikuta akianguka polepole huku Profesa Chain akimtazama kwa kicheko cha kebehi. Hakuwa na uwezo wsa kupiga kelele japo alijaribu, akahisi fahamu zikimtoka taratibu.
ITAENDELEA 0784296253

Comments
Post a Comment