WACHEZAJI STARS WALIKOSA UBUNIFU

Kwa mara nyingine, watanzania wamepoteza furaha baada ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kufungwa mabao 2-0 na Mafarao wa Misri, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa, Stars chini ya nyota Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu (wanaoonekana katika picha juu) walitakiwa kushinda mchezo huo kwa mabao 2-0, ili kufikisha pointi nne na kubakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Nigeria ambao hawakuwa na nafasi yoyote, baada ya kuambulia pointi mbili,  kwa michezo mitatu, ambapo walitoka sare ya 1-1 na Mafarao nchini Nigeria, 2-2 dhidi ya Tanzania Uwanja wa Taifa na kuambulia kichapo cha 2-0 Misri.

Wachezaji wa Stars waliokuwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo, walionekana kukosa mbinu na pengo la mabeki Nadri Haroub 'Canavaro' na Kelvin Yondan lilionekana wazi na kuchangia kwa kiasi kikubwa, mchezaji wa Misri Mohamed Salah (pichani chini), kufunga kwa urahisi, moja kwa mkwaju wa adhabu ndogo na lingine kwa kumzidi ujanja Haji Mwinyi Ngwali.

Agrey Moris aliyekuwa mlinzi wa kati alionekana wazi kukosa umakini hata wakati wa kupanga safu ya ulinzi wakati wa kupiga faulo. Washambuliaji Samata na Ulimwengu pia hawakuwa makini kuliona lango la Misri pamoja na kupata nafasi nyingi za kufunga ikiwemo penati walikosa kuleta furaha kwa watanzania.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru