WATANZANIA WAFURAHIA KUPATA HABARI ZA HARAKA NA UHAKIKA KUPITIA MITANDAO

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Hassan Abbas (katikati) akizungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Blooggers Network uliofanyika Dar es Salaam hivi karibuni. Mkutano huo wa siku mbili ulihudhuriwa na wamiliki wa Mitandao ya Kijamii kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania ukiwa na kauli mbiu “Mitandao ya Kijamii ni Ajira, itumike kwa Manufaa”.

Na Nyakasagani Masenza Dar es Salaam

Siku chache baada ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Moses Nnauye kufunga rasmi Mkutano  Mkuu wa Mwaka wa wamiliki wa Mitandao ya Kijamii, Tanzania Blooggers Network kama inavyoonekana katika picha, uliofanyikawa Dar es Salaam, Baadhi ya wadau wanaopata habari kupitia mitandao hiyo wameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali kuitambua.

Wakizungumza na Mwandishi wa MPIGANAJI Dar es Salaam leo, wadau hao wamesema, kupitia Mitandao ya Kijamii, wananchi wanapata habari haraka tofauti na vyombo vingine vya habari.

Kinyami Mwitazi wa Vingunguti, amesema kila wakati yeye huingia kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii kuangalia taarifa zilizotokea,  Anasema kupitia mitandao hiyo amekuwa akiangalia taarifa za habari za usiku na kusoma magazeti ya kesho akiwa na taarifa za yaliyotokea.

"Mitandao ya Kijamii imerahisishia jamii kupata taarifa za haraka", anaeleza Kinyami huku akishauri Serikali kusaidia waandishi wa mitandao hiyo ili waongeze kasi ya kuhabarisha jamii.

Tigani Nyakire, akawataka waandishi wa Mitandao kuandika sana habari za vijijini. Anasema wanandchi wengi wa vijijini bado hawana ufahamu kuhusu mitandao ya kijamii, iwapo serikali itasaidia kutoa elimu kwa wananchi hao mitandao itawasaidia kupata habari za haraka tofauti na sasa ambapo sehemu zingine za nchi wanasoma magazeti baada ya siku mbili na zaidi.

 Mdau mwingine wa Mitandao ya Kijamii, China Kilinda, aliipongeza Serikali, hususan Waziri mwenye dhamana na habari, kuwa mikakati yake ya kuboresha mitandao hiyo itasaidia kwa kiasi fulani kufikisha habari za uhakika karibu zaidi kwa wananchi wengi
  Baadhi ya Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Blooggers Network uliofanyika Dar es Salaam
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Blooggers Network wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mafunzo kwa wanachama hao yaliyofanyika Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA BENJAMIN SAWA)

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU