YANGA, SIMBA NI VITA VYA KARNE

 KIKOSI CHA YANGA
 KIKOSI CHA SIMBA 
 Mshambuliaji hatari wa Klabu ya Yanga, Amis Tambwe akishangilia moja ya magoli aliyoifungia timu yake ya Yanga
 Mshambuliaji tegemeo wa Klabu ya Simba Laudit Mavugo, akishangilia moja ya magoli aliyoifungia timu yake ya Simba. 

Ni vita ya mafari wawili unaweza kusema, ili ubishi uishe ni lazima dakika 90 zitumike kuamua nani mbabe. Hakuna ubishi tena Klabu kongwe nchini zenye upinzani wa Jadi katika soka la Tanzania Yanga na Simba lazima zikutane kesho kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo huo umekuwa na hamasa kubwa kutokana na timu hizo kukabana vilivyo toka msimu wa pili uanze, Yanga wakishika usukani kwa muda na kisha Simba kuukalia tena, lakini wapinzani wao Yanga wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Kuelekea mchezo huo mengi yamesemwa na wengine kuomba dua kwa baadhi ya wachezaji wanaodaiwa kuwa majeruhi waendelee kuwa majeruhi ili mradi tu wasicheze mchezo kutokana na ubora wao.

Mshambuliaji mwenye nguvu wa Yanga, Donald Ngoma amekuwa gumzo kubwa nchini Tanzania, kiasi cha kumfanya Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage kumuombea mabaya mchezi huyo aendelee kuwa majeruhi ili asicheze mchezo huo. 

Pamoja na figisu hizo Uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa Ngoma ni majeruhi na hawezi kutumika katika mchezo huo. Hata hivyo wamejinasibu kuwa ushindi ni lazima kwani Yanga inao washambuliaji wengine kama Obrey Chirwa, Simon Msuva, Amis Tambwe na Deus Kaseke.

Simba nao wanaonekana kuwa na washambuaji wenye kasi kama Laudit Mavugo. Ibrahim Ajibu na Shiza Kichuya, wametamba kuwa lazima kieleweke ili waendelee kuukaria usukani wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kutokana na ushindani kuwa mkali, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limelazimika kuficha majina ya waamuzi wa mchezo huo wakidai kuwa kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu waamuzi. Msemaji wa Shirikisho hilo, Alfred Lukas amesema TFF imeteua majina ya waamuzi wanne wa kati ambao kila mmoja amepewa taarifa za kuchezesha mchezo huo lakini lolote laweza kutokea.

Nani ataibuka mshindi, dakika 90 zitakapokwisha ndipo mashabiki wa timu hizo wataelewa nani mbambe na nani kibonde. Ili ubishi uishe ni lazima miamba hiyo ikutane katika raundi ya pili, Simba wakiongoza kwa pointi 51 mbele ya Yanga yenye pointi 49.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru