HABARI ZA HIVI PUNDE; MCHUNGAJI GWAJIMA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA YA KISUTU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam imemwachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat 
Gwajima (pichani kushoto) aliyekuwa akikabiliwa na shitaka la kutumia lugha chafu ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar eses Salaam, Mwadhama Polycapry Kadnali Pengo.

Askofu Gwajima ameachiwa huru leo chini ya kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa kesi za Makosa ya jinai (CPA). Baada ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Bw. Cyprian Mkeha, kubaini kuwa upande wa mshitaka wameshindwa kuleta mashahidi kwa takriban miaka miwili.

Awali kabla ya kufutwa kwa kesi hiyo, Mwanasheria wa Serikali Joseph Maugo, aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba hawana shahidi na hivyo kuiomba mahakama kuahirishwa tena kwa kesi hiyo.

Kufuatia maelezo hayo ya Mwanasheria wa Serikali, Hakimu Mkeha, amesema kwa muda wa miezi 14 sasa upande wa mashitaka umeweza kuleta shahidi mmoja pekee, jambo ambalo ameserma linaonesha wazi kuwa pande wa mashitaka hauna shahidi mwingine hivyo anaifuta kesi hiyo.

Katika shauri lililopita, mahakama iliutaka upande wa mashitaka kuhakikisha inaleta mashahidi kwa ajili ya kuendelea na kesi hiyo lakini kwa muda wote huo hawakutimiza masharti.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kati ya Machi 16 na 25 mwaka jana, huko eneo la Tanganyika Packers Kawe, Dar es Salaam, Askofu Gwajima alitumia lugha chafu ya matusi dhidi ya Askofu Pengo.

Ilibainishwa kuwa Askofu Gwajima alimtukana kwa kumwita Askofu Pengo kuwa ni Mpuuzi mmoja, mjinga mmoja asiyefaa mmoja anaitwa Askofu Pengo aliropoka sijui amekula nini, mimi naitwa Gwajima, namwita mpuuzi yule mjinga yule na kuonesha kuwa Askofu Pengo ni mpuuzi na mwenye akili ndogo na kwamba maneno hayo yangeweza kuleta uvunjifu wa amani.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU