KOMBE LA DUNIA KUONYESHWA MUBASHARA DSTV


SuperSport imethibitisha kuwa ni kitovu cha burudani hususan ya soka baada ya kukamilisha makubaliano makubwa na shirikisho la soka la dunia FIFA ikiwemo kurusha kombe la dunia mwaka 2018 mubashara. Michuano hiyo itafanyika nchini Urusi

Burudani ya  soka kwa wateja wote wa DStv itakuwa ya aina yake kwani mechi zote 64 zitaonyeshwa mubashara kwenye mgumo wa High Definition, hii ikimaanisha kuwa wateja wa DStv watauona mtanange huo katika muonekano bora zaidi.

Makubaliano mengine yaliyofikiwa kati ya SuperSport na FIFA ni pamoja na urushwaji wa matangazo ya Kombe la dunia la timu za umri wa chini ya miaka 20 maarufu kama U-20 pamoja nay ale ya wachezaji wa wenye umri wa chini ya miaka 17 yaani U-17. Mashindano mengine ambayo yatarushwa na SuperSport ni pamoja na Kombe la dunia la soka la ufukweni  pamoja na kombe la dunia la U-20 na U17 kwa wanawake.

Makubaliano haya yanaendelea kuifanya SuperSport kuwa gwiji kwenye kutoa burudani hususan soka ukizingatia kuwa bado wanaendelea kurusha ligi maarufu duniani kama ile ya Uingereza , Hispania, Afrika Kusini na kadhalika.

“Kandanda ni lulu kwenye SuperSport” anasema Mkurugenzi Mkuu Gideon Khobane. “tumekuwa kukifurahia burudani ya kombe la dunia kwa miaka mingi na kwa makubaliano haya ya sasa tuna uhakika wa kuendelea kuwapa wateja wetu burudani zaidi. Cha msingi, wateja wetu wategemee burudani ya kiwango cha juu”. 


SuperSport has confirmed itself as Africa’s home of world football after completing a broadcast deal with FIFA for its major international rights for the 2017/18 season.

DStv customers’ football experience will be taken to a whole new level with the impending FIFA Confederations Cup in Russia and the FIFA World Cup, which also takes place in Russia in June 2018. All 64 matches will be broadcast live in High Definition.

Other FIFA events on the broadcast calendar are the FIFA Under-20 and Under-17 World Cups, the FIFA Beach Soccer World Cup and, in 2018, the FIFA Under-20 and Under-17 Women’s World Cup tournaments.

These acquisitions now sit alongside SuperSport’s already substantial offering that includes the major leagues, Champions League and the SA Premier Soccer League.

“Soccer is among the jewels in the SuperSport crown,” said Gideon Khobane, SuperSport Chief Executive. “We have long enjoyed the thrills of the World Cup and FIFA’s other properties and this new arrangement prolongs what has become a great partnership.”

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru