WINGA BARUAN AKILIMALI ANASA ANGA ZA YANGA

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Klabu ya YANGA AFRIKA imefanikiwa kumsajili kiungo chipukizi, Baruan Yahya Akilimali (pichani kushoto), aliyekuwa anasoma nchini Uganda kwa mkataba wa miaka miwili.

Winga huyo teleza wa kulia anayeweza kucheza pia upande wa kushoto, amesaini kwa mkataba wa miaka miwili kujiunga na wana Jangwani hao. huku
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akisema kwamba wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo kwa muda mrefu kabla ya kuridhishwa naye na kuamua kumsajili.

Baada ya kuonyesha kipaji kikubwa katika mashindano ya shule za sekondari Uganda mwaka juzi, mdogo huyo wa winga wa zamani wa Simba, Akilimali Yahya alishawishiwa kuchukua uraia wa nchi hiyo ili achezee timu ya vijana ya taifa hilo, The Kobs, lakini Baruan akakataa.

Yanga wanaamini Baruan atakuwa mrithi wa Simon Happygod Msuva aliye mbioni kujiunga na timu ya Ligi Kuu nchini Morocco, Difaa Hassani El-Jadida, ambayo inamchukua yeye na Mtanzania mwingine, winga pia Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Azam FC.

Timu hiyo yenye maskani yake mji wa El Jadida ikiwa inatumia Uwanja wa El Abdi inataka kujaribu kutwaa taji la Ligi Kuu ya Morocco, inayojulikana kama Botola, moja ya Ligi bora kabisa barani Afrika. Baruan Yahya Akilimali aliyekuwa anasoma nchini Uganda amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

HOFU

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru