MULTICHOICE TANZANIA YAJA NA OFA YA SIKUKUU


Dar es Salaam Jumanne November 21, 2017; Kama ilivyo ada, katika msimu huu wa sikukuu, Multichoice Tanzania imetangaza neema kwa watanzania kwa kutoa ofa kabambe kwa wateja wake ambapo kuanzia leo mteja mpya wa DStv ataweza kuunganishwa kwa shilingi 79,000 tu kwa vifaa vyote pamoja na kifurushi cha DStv Bomba cha mwezi mzima.

Akizungumzia ofa hiyo, kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo, amesema kuwa Multichoice imekuwa na utamaduni wa miaka nenda rudi wa kuwapa zawadi wateja na watanzania kwa ujumla na kwamba kila ufikapo msimu kama huu DStv huwatunuku wateja wake ili kuwawezesha kufurahia zaidi msimu wa sikukuu.

"Tunafahamu kuwa msimu huu wa sikukuu familia nyingi zinaungana katika kusherehekea, hivyo DStv imeamua kuwaongezea burudani kwa kutoa ofa hii kabambe". Amesema badala ya mteja mpya kulipa shilingi 98,000 kwa ajili ya kuunganishwa pamoja na kifurushi cha mwezi, sasa wateja wapya watalipa shilingi 79,000 tu na kuunganishwa na DStv pamoja na kifurushi cha Bomba cha mwezi mzima.

“Tunapokuwa nyumbani na familia zetu, watoto wanataka waangalie katuni, sisi kinamama tunapenda kuangalia vipindi kama vile vya mapishi, urembo, na tamthilia, kinababa nao hupenda sana kutazama michezo mbalimbali kama kandanda na kadhalika. Ni kwa msingi huu tumeamua kuwarahisishia burunani hii inayopatikana kutoka DStv” alisema Hilda na kuongeza kuwa wataendelea kutoa ofa kwa wateja wao kila inapihitajika. Ofa hii ni kwa nchi nzima na itaendelea kwa miezi miwili hadi Januari 15, 2018

Hilda amesema Ofa hii kwa wateja wapya inakuja siku chache tu baada ya DStv kuanza kutoa zawadi kwa wateja wake kwa kuwaongezea chaneli za SuperSport kwenye vifurushi vyao punde walipiapo akaunti zao kabla hazijakatika. Katika ofa hii ya kuongezewa chanel, wateja wa kifurushi cha Compact na Compact Plus watapata chaneli zote za SuperSport zinazopatikana katika kifurushi cha DStv Premium kwa kipindi cha siku saba (7) mfululizo bureeee!

Hali kadhalika, watumiaji wa  kifurushi DStv Bomba  na DStv Family  nao watapata chanel zote za Supersport zinazopatikana kwenye Kifurushi DStv Compact na hivyo kuweza kushuhudia mechi zote za Ligi ya Uingereza (PL) na mashindano mengine makubwa kwa siku saba (7) mfululizo bureee! Multichoice Tanzania imekuwa ikitoa huduma za DStv hapa nchini kwa Zaidi ya miaka 20 sasa na imeendelea kuwa kinara katika kuwapatia watanzania habari, elimu na Zaidi ya yote burudani kabambe.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU