TPB YAUNGANA NA MULTCHOICE KUKOPESHA DStv

Benki ya Posta Tanzania (TPB) imeingia kwenye makubaliano rasmi na kampuni ya Multichoice ambapo wafanyakazi, wateja na hata wale wasio wateja sasa wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo.

Kwa makubaliano hayo watanzania wengi wanaotaka kumiliki ving’amuzi vya DStv, sasa watapata mkopo maalum kutoka Tpb utakaowawezesha kufungiwa huduma za DStv na kulipa kwa awamu kati ya miezi mitatu hadi mwaka mzima.

Akizungumza wakati wa kutangaza rasmi makubaliano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi, amesema kuwa benki yake siku zote imekuwa ikijitahidi kubuni huduma mbalimbali kwa ajili ya kuwafanya watanzania wengi kupata huduma muhimu na pia katika kuboresha hali zao ki uchumi na kijamii.

Amesema kuwa wameamua kuingia kwenye makubaliano na kampuni ya Multichoice ili kuwapa fursa wafanyakazi na wateja wa benki hiyo waweze kupata huduma muhimu za DStv kwa mkopo, hii ikimaanisha hawatalazimika kulipa fedha yote kwa mkupuo mmoja badala yake watakuwa wanalipa kwa awami kadhaa. 

“Benki yetu ni benki ya watanzania wa kada zote, na wenzetu wa Multichoice nao hali kadhalika, sasa tumeamua tuungane ili tuwawezeshw ndugu zetu watanzania kupata fursa ya kuwa na huduma ya DStv kwa njia ambayo ni rahisi kwao” alisema  Moshingi.

“Leo hii tumeongeza wigo wa mikopo tunayoitoa, ambapo sasa Mtanzania ataweza kufurahia zaidi kwa kupata kinga’muzi cha DStv na hivyo kwenda sambamba na ulimwengu wa Kisasa kwa kupata habari za kila aina kwa wakati”. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande amesema Multichoice imekuwa wakati wote ikiwasikiliza wateja watanzania na kuhakikisha inawafikishia huduma zake kwa njia rahisi Zaidi.

Amesema makubaliano haya na Tpb ambayo ni moja ya benki madhubuti hapa nchini yatawawezesha watanzania wengi kupata huduma mbalimbali muhimu kama vile za televisheni kwa urahisi Zaidi. “Tunafahamu kuwa Tpb ina ni benki kongwe na ina mtandao mkubwa hapa nchini na hivyo ushirikiano wetu utatuwezesha kuwafikia watanzania wengi kila pembe ya nchi” alisema Maharage.

Amesisitiza kuwa Multichoice, kwa king’amuzo chake cha DStv, imekuwa mstari wa mbele katika kuwapatia watanzania habari na burudani na huduma hizo zimekuwa moja ya mahitaji muhimu ya watanzania kwani kwa kuptita DStv, sasa watanzania wanaenda sambamba na ulimwengu mzima kwenye kupata habari mbalimbali za kiuchumi, kisiasa, utamaduni, Sanaa michezo na burudani.

Kwa makubaliano haya kati ya Ypb na Multichoice Tanzania, Wtatnzania watapata kirahisi mikopo ya ving’amuzi vya Dstv kupitia matawi yote ya Tpb kote nchini ambapo mteja atapatiwa kinga’muzi, dishi, kifurushi cha kuanzia pamoja na gharama zote za ufundi na kisha kulipa kwa muda atakaotaka ikiwa ni kati ya miezi mitatu hadi mwaka mzima.

Mkopo huu wa kupata king’amuzi cha DStv, unaanza maramoja, na ili kuhakikisha watanzania wengi wananufaika, vigeza na masharti vilivyowekwa vimezingatia hali halisi yam Tanzania.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU