MAMS BAKER WATESA AZAM CAKES AND BREAD EXPO

Mkurugenzi Mkuu wa Mams Baker, iliyoko Jengo la Benjamin Mkapa Tower, Bi. Pili Mpenda (kushoto), akitoa maelekezo kwa wasaidizi wake wakati wa maonyesho ya Azam Cakes and Bread Expo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Leades Klabu Dar es Salaam jana.. Mams Baker waliibuka washindi wa kwanza. 

Mams Baker Bites walioko katika jengo la Benjamin Wiliam Mkapa Tower, ambao ni watengenezaji wa Cakes na Bites bora na tamu kabisa, jana waliibuka kidedea wakati wa maonyesho maalum ya kujitangaza, kubadilishana uzoefu na Kujenga Mtandao wa pamoja wa wana fani (NETWORKING) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Leaders Klabu Jijini Dar es Salaam.

Katika Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Azam, yakijulikana kama Azam Cakes and Bread Expo, Mams Baker ambao pia wana tawi pale Governors ADA Estete waliibuka washindi wa kwanza wa kutengeneza mikate. Pia waliibuka washindi wa pili wa Display na kushinda tena nafasi ya tatu wa  Peoples Choice za test za keki baada ya mashabiki kuonja na kuwapigia kura.

Akizungumza kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi kwanza katika maonyesho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Mams Baker, Pili Mpenda amesema ushindi huo umetokana na jitihada zao binafsi. amesema uongozi na wafanyakazi wamefurahishwa sana na ushindi huo ambao utawaongeza chachu ya kufanya vizuri kwa ufanisi zaidi.

"Bidhaa zetu ni bora, tulijiamini tukijuwa tutashinda, kwanza tunajituma kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma nzuri, tumejipanga vizuri na wafanyakazi wote wa City Center Bites kuhakikisha tunatoa huduma bora. ili kuhakikisha tunatoa huduma hii vizuri tunapatikana kuanzia saa 12:30 asubuhi mpaka saa 2:30 usiku", amesema.

Mkurugenzi huyo wa Mams Baker amewataka watanzania hususan wanaopenda vitu vizuri kuwasiliana nae kwa namba 0716838260 au 0687868980, na kwamba Mams Baker wapo katika Jengo la Benjamin Mkapa zilipo ofisi za NSSF wakiangaliana na duka la nguo la Mariedo Fashion. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mams Baker, Pili Mpenda (wa pili kulia) akiwa na wasaidizi wake wakionyesha baadhi ya bidhaa zao wakati wa maonyesho ya Cake, kwenye viwanja vya Leaders Klabu, Dar es Salaam jana
Watoa huduma wa Mams Baker wakiandaa bidhaa kwa ajili ya mashindano ya Azam Cakes and Bread Expo jana.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mams Baker, Pili Mpenda (kushoto) akitoa maelekezo kwa wasaidizi wake wakati wakijiandaa na maonyesho ya Cake ya Azam Cakes and Bread Expo, kwenye viwanja vya Leaders Klabu, Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Mams Baker waligawa cake na Bites kwa watu mbalimbali wakati wa mashindano ya AzamCakes and Bread Expo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mams Baker Pili Mpenda (kulia) akisaidiana na Fatuma Kinega kuandaa baadhi ya mikate kwa ajili ya mashindano ya AzamCakes and Bread Expo jana.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU