SUPER SPORT KUONYESHA LIGI YA MABINGWA

Magwiji wa kuonyesha michezo kote barani Afrika – SuperSport imethibitisha rasmi kuwa imepata idhini ya kuonyesha moja ya michuano maarufu kabisa ya soka ulimwenguni -  Kambe la UEFA ambapo sasa michuano hiyo itaonekana mubashara kupitia DStv na hivyo kuwawezesha mamilioni ya watazamaji kote barani Afrika kushuhudia michezo hiyo.

Hivi karibuni, SuperSport ilishiriki katika zabuni ya kupata idhini ya kuonyesha michuano hiyo na hatimaye kuthibitisha kupata idhini ya kuendelea kuonyesha michuano hiyo kwa miaka mitatu ijayo kuanzia msimu wa 2018/19.

“Hii ni siku ya Furaha na muhimu sana kwa SuperSport na wateja wetu wote wa DStv” amesema Mtendaji Mkuu wa SuperSport Gideon Khobane na kuongeza kuwa michuano ya UEFA ni moja ya mashindano makubwa Ulimwenguni na yanayoshirikisha timu maarufu na wachezaji wengi nyota".

Gideon Khobane amedokeza kuwa kuonekana kwa michuano hii itakuwa ni moja ya burudani za aina yake kwa watazamaji wa DStv kote barani Afrika. Amesema kama kawaida, kupitia DStv, watazamaji wataona michuano hiyo mubashara tena kwa muonekano wa kiwango cha juu.

Idhini waliyopata SuperSport ni pamoja na kurusha matangazo yake kwa njia ya Televisheni, simu na kupitia internet kwa ujumla.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU