YANGA WATAMBA KUTWAA TENA UBINGWA 2018

Baada ya kuwatambia Azam kwenye uwanja wao wa nyumbani Chamazi kwa kuwachakaza kwa magoli 2-1, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Dar es Salaam Yanga Afrika (pichani juu) wamejinasibu kuwa pamoja ya kuwa nyuma kwa pointi saba dhidi ya mahasimu wao Simba watautwaa ubingwa wa Ligi hiyo msimu huu.

Yanga ambao mara kadhaa wamekuwa na kawaida ya kusuasua katika mzunguko wa kwanza na kuzinduka raundi ya pili kama msimu uliopita, wametamba kuwa nyuma kwa pointi saba za Simba si lolote kwao kwani ligi kuu bado haijaisha.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema hii si mara ya kwanza kwa Simba kuongoza Ligi kwa idadi pointi lakini Yanga wamekuwa wakifanya vizuri katika mzunguko wa pili na kutwaa ubingwa. Amsema msimu uliopita Yanga walikuwa nyuma kwa pointi nane lakini leo Yanga ndiye bingwa mtetezi.

"Mchezo wa soka ni sawa na mbio za nyika, wakimbiaji dhaifu hukimbia haraka ili waweze kuongoza lakini wanapofika kwenye milima huanza kuishiwa pumzi na hatmaye kupitwa, Yanga tumekuwa na kawaida ya kuanza vibaya lakini ubingwa unatuhusu", amesema Mkwasa ambaye pia amewahi kuwa mchezaji wa Klabu hiyo na kushika nyadhifa mbalimbali pia.

Ili kuthibitisha kuwa Yanga wanatwaa tena ubingwa msimu huu Jumamosi iliyopita wakicheza kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi waliweza kuvunja mwiko wa Azam ambao hawajawahi kufungwa katika uwanja wao. Azam walishindwa kutumia vyema Uwanja wa nyumbani baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 28 baada ya kucheza michezo 15, wakiendelea kubaki nafasi ya tatu, nyuma ya Azam enye pointi 30. Simba bado wanaongoza ligi hiyo kwa point 35 baada ya jana kuikausha Majimaji ya Songea kwa mabao 4-0 katika mchezo wa mwisho wa rmzunguko kwa kwanza uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo wa Yanga na Azam ulichezeshwa na Israel Mujuni Nkongo aliyesaidiwa na washika vibendera Soud Lila na Frank Komba, hadi mapumziko Yanga walikuwa wamekwishatengeneza ushindi wao huo baada ya Obrey Chirwa kufuta bao la Bruce Kangwa na Kinda Gadiel Michael kuihakikisha Yanga ushindi kwa shuti la mbali lililomshinda kipa wa Azam, Razak Abarola.
 Kikosi cha Azam kilichoshindwa kufurukuta mbele ya Yanga Chamazi
 Beki chipukizi wa Yanga Gadiel Michael akiubusu uwanja wa Chamazi baada ya kuachia fataki lililomshinda kipa wa Azam Razak Abarola na kutinga wavuni kuandika bao la pili. Wengine kutoka kushoto ni Papii Kabamba Tshishimbi, Andrew Vicent, Obrey Chiorwa, Ibrahim Ajib na Raphael Daud.
 Bruce Kangwa wa Azam akijaribu kumtoka mlinzi wa Yanga, Hassan Kesy
Kevin Yondan akiruka juu kuokoa unaonyemelewa na mshambuliaji wa Azam Shaaban Iddi
 Kiungo wa Yanga, Raphael Daudi akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Azam FC
 Juma Mahadhi akimtoka kiungo wa Azam, Himid Mao aliyecheza kama beki wa kulia
Papy Kabamba Tshishimbi akiondoka na mpira huku akiangaliwa kwa makini na mshambuliaji wa Azam, Mbaraka Yussuf 
Obrey Chirwaaaaaaaa PICHA ZOTE KWA HISANI YA BIN ZUBERY)

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU