MULTICHOICE TANZANIA YAZINDUA KITUO MWANZA

 Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo maalum cha huduma jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Kanda John Kasuku

Katika kuhakikisha kuwa inaimarisha na kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja, kampuni ya MultiChoice Tanzania imefungua kitua kipya cha huduma  jijini Mwanza.
Kituo hicho kilichofunguliwa mwishoni mwa wiki ni muendelezo wa mkakati wa kampuni hiyo kuwasogezea wateja wake huduma karibu ambambo hivi karibuni, kituo kama hicho kilifunguliwa mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo amesema kituo hicho ni cha Kisasa na kinaweza kuwapa wateja wa DStv huduma zote kuanzia kununua vifaa, kufanya malipo, ufundi na huduma kwa wateja. 

Amesema huu ni mkakati maalum wa MultiChoice Tanzania kufungua vituo kama hivyo kote nchini ambapo hivi karibuni  vituo zaidi vitafunguliwa katika miji ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Dodoma.

Hivi sasa mkakati wetu mkubwa ni kuhakikisha kuwa mteja aliyeko mkoani anapata huduma sawasawa na yule aliyepo Dar es Salaam kwani vituo hivi vya huduma vimeboreshwa na kuwa na uwezo wa kutoa kila aina ya huduma alisema Shelukindo.

Amewataka wateja wa DStv jijini Mwanza kukitumia kituo hicho kwa ufanisi na pia sasa kampuni hiyo pia inaimarisha timu yake ya mauzo, kuongeza idadi ya mawakala ili kuhakikisha kuwa wateja wanahudumiwa kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa.

Kuhusu changamoto za kiufundi, Shelukindo amesema hili sasa limepatiwa ufumbuzi kwani MultiChoice imetoa mafunzo maalum ya ufundi kwa mamia ya vijana kote nchini kwa ajili ya kuwahudumia wateja wake. Amesema kuanzia sasa kutakuwa na mafundi maalum walioidhinishwa ambao wamepatiwa mafunzo maalum. 


 Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo akitoa maelezo kuhusu kituo maalum cha huduma jijini Mwanza mara tu ya ufunguzi wa kituo hicho mwishoni mwa wiki. 


 Meneja wa Kanda ya Ziwa wa MultiChoice Tanzania John Kasuku (kulia) akimkabidhi muandishi wa habari George Ramadhani seti ya DStv baada ya muandishi huyo kuwa miongoni mwa waandishi waliojishindia seti ya DStv wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha huduma jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU