YANGA WAAPA NA KUAZIMIA KUFA KIUME

Mabingwa wa kihistoria na wababe wa muda mrefu wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Dar Yanga Afrika wameapa na kuahidi kuwa watapigana kufa na kupona kuhakikisha wanautwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu wa 2020- 2021. 

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Mshindo Msola na Nahodha wa zamani wa timu hiyo Haruna Niyonzima wamebainisha kuwa iwe juwa inyeshe mvua watambana kuhakikisha wanapata matokeo mzuri kwa michezo tisa iliyosalia.

Jana ikicheza na Biashara United ya Mara, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 lililopachikwa wavuni na mshambulia wake Yaucuoba Signe wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Baada ya mchezo huo Yanga imejiweka sawa kuwakabiri Gwambina kutoka Misungwi Mwanza, mchezo utakaochezwa Jumanne kwenye uwanja huo wa Mkapa. Hata hivyo Yanga wasitegemee kupata ushindi kutokana na aina ya uchezaji wa Gwambina ambao katika mchezo wa kwanza walitoshana nguvu kwa kutoka suruhu.

Katika raundi hii ya lala salama, Yanga watatoka nje ya Dar es Salaam mara tatu, moja watakuwa kwenye uwanja wa Majaliwa Ruangwa kusaka pointi tatu kwa Namungo na Jamhuri Dodoma kwa ajili ya kusaka pointi kwa JKT Tanzania na Dodoma Jiji.

Michezo ambayo Yanga watakuwa Dar es Salaam ni kati ya mahasimu wao Simba, Gwambina, Azam, Ruvu Shooting, Mwadui na Ihefu. Hata hivyo Yanga wanaweza kuwa mabingwa msimu huu iwapo wpinzani wao Simba watapoteza michezo mitatu nao washinde iliyobaki.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU