Matukio mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam katika picha


Basi la abiria 'Daladala', T 198 ACB, likining'inia kwenye ukingo wa Barabara, baada ya kunusurika kuanguka ndani ya shimoa likiwa na abiria, dereva wake aliposhindwa kupanda mlima, eneo la BP, Dar es Salaam. Hakuna aliyejeruhiwa.
 Mlemavu wa viungo akiwa amekaa katikati ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kwenye taa za Usalama za Ubalozi, wakati akiomba msaada kwenye magari, Dar es Salaam, kitendo ambacho ni hatari kwa usalama wake.

Mwanasheria anayewakilisha wanunuzi wa nyumba zilizokuwa za shirika la Bandari, zilizoko eneo la Gerezani, Dar es Salaam, Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto), akizungumza na wateja, kuhusu maendeleo ya kesi yao ya Ardhi.
 Wabeba takataka wa Manspaa ya Ilala, wakiwa wameegesha gari lao katikati ya Barabara ya Msimbazi, Dar es Slaam, wakati wakikusanya takataka hizo, kwa ajili ya kuiweka manispaa hiyo katika hali ya usafi.
 Mfanyabiashara ndogo ndogo, akiandaa vitunguu na bidhaa nyingine za kuwauzia wateja wake, kama alivyokutwa na kamera yetu eneo la Soko kuu la Kariakoo, Dar es Salaam.

Katika kuadhimisha Sikukuu za Krismasi na mwaka mpya, Father Christmas’ wa Kampuni ya FK Motos LTD, juzi aligawa zawadi za Sikukuu kwa watoto, wakati wa Uzinduzi wa gari mpya aina ya Kia Sportage iliyotengenezwa Korea, kwa ajili ya mwaka 2012, kwenye Viwanja vya Mlimani City Dar es Salaam.

Comments

HABARI ZILIZOPITA

HEKAYA ZA ABUNUWASI

HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79

PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru

HOFU