Hili ndio Daraja la kisasa la Kigamboni, lililoko eneo la Kurasini, Manispaa ya Temeke, Jijini Dar es Salaam. Daraja ambalo wahandisi wanasema litazinduliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete, Oktoba Mwaka huu kabla ya hajastaafu nafasi hiyo.
Meneja Mradi
wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Mhandisi Karim Mataka (kushoto), akionyesha sehemu ya mradi wa daraja
hilo kwa Makamishna kutoka Bunge la Nigeria, Bi. Barr Lamnye (kulia), Alhaj
Aliyu Abubakar (wa pili kulia) na Kiongozi wa msafara huo Bw. Elder Stephen Yepwi, walioko nchi kwa
ziara ya kikazi.
Mhandisi Karim Mataka kutoka NSSF (wa pili kulia), akiwaelekeza jambo Makamishna wa
Bunge la Nigeria, Bw. Elder Stephen Yepwi (wa tatu kushoto) na Alhaj Aliyu
Abubakar (wa pili kushoto), walipotembelea ujenzi wa daraja hilo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mhandisi Mohamed Abdepbay na Mhandisi Liu Too (kushoto).
Kiongozi wa msafara wa Makamishna wa Bunge la Nigeria, Bw. Elder Stephen Yepwi (wa pili
kulia), akifafanua jambo kwa Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni,
kutoka shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mhandisi Karim Mataka (wa
pili kushoto), baada ya Makamishna wa Bunge la Nigeria kutembelea daraja hilo,
Dar es Salaam leo.
Wakijadiliana jambo baada ya Wabunge hao kuvutiwa na mradi huo mkubwa.
Hili ndio Daraja la kisasa la Kigamboni.
Hii ni Barabara Kuu inazotoka kwenye Daraja la Kigamboni, kwa ajili ya kuungana na barabara Kuu ya Mandela, ikiwa katika hatua ya mwisho
Hii ni sehemu ya Daraja la Kigamboni ambayo ujenzi wake umekamilika.
Kipande cha Daraja la Kigamboni kinachosubiri kuuganishwa na njia kuu.
Meneja Mradi
wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Mhandisi Karim Mataka akizungumza na Makamishna hao baada ya kutembelea mradi huo, Dar es Salaam leo.
Comments
Post a Comment