Posts
- Get link
- X
- Other Apps
HABARI ZILIZOPITA
HEKAYA ZA ABUNUWASI
HEKAYA ZA ABUNUWASI ni kitabu cha hadithi za kusisimua, zinazofurahisha sana kutokana na umahili wa watunzi wa vitabu vya kale. Kutokana na utamu wa hadithi za ABUNUWASI, Blog ya MPIGANAJI itawaletea hadithi hizo ili kuwachangamsha akili............... KISA CHA ABUNUWASI NA MFALME SIKU moja alfajiri, wakati wananchi wa mji wenye wakazi wengi walipokwenda kuchota maji mtoni, walishangazwa kuuona mkono wa mtu ukiwa katikati ya mto. Mkono huo wa ajabu ulikuwa umenyoosha vidole viwili juu, kuonyesha alama ya mbili. Wananchi walistushwa sana na kitendo hicho, wakaogopa hata kuchota maji mtoni, kwani hawakuwahi kuona tukio la kuogopesha kama lile. Wengine waliamini kuwa huo ulikuwa mwili wa mtu aliyetupwa mtoni. Lakini ishara iliyoonyeshwa na mkono huo iliwafanya wananchi waamini kuwa huo ulikuwa mkono wa ajabu. Katika kiza kinene kilichozunguka ndani ya vichwa vya wananchi, habari zikamfikia Mfalme wao, naye akafika haraka eneo la tukio. Mfalme wa nchi hiyo baada ya kujiridhisha k
HISTORIA YA VITA VYA KAGERA 1978 - 79
MAJESHI YA UGANDA YALIVYOINGIA KAGERA MWAKA 1978, Majeshi dhalimu ya Nduli Idi Amin Dadaa wa Uganga, yalivamia Ardhi ya Tanzania, eneo la Mto Kagera, katika mkoa wa Ziwa Magharibi na kufanya uharibifu mkubwa wa mali na kuua wananchi wa mkoa huo, NYAKASAGANI MASENZA anasimulia kupitia vyanzo mbali mbali vya habari jinsi majeshi hayo yalivyoingia Tanzania na Amin kutangaza rasmi kuwa eneo hilo la Mto Kagera ni sehemu ya Uganda. DAIMA Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa ukombozi wa Bara la Afrika, ikiwa miongoni mwa mataifa masikini zaidi duniani, lakini iliyojariwa viongozi wenye hekima, kuanzia muasisi wake Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete. Busara za viongozi wa Tanzania zilianza kuonekana mwaka 1961, baada ya Mwalimu Nyerere kuwanasua watanzania kutoka mikononi mwa utawala kandamizi wa wakoloni, wakati huo pia akiwa tayari kuchelewesha Uhuru wa Tanganyika ili nchi zingine zilizokuwa kwenye mchakato wa uhuru zipa
PATA HADITHI ZA UPELELEZI ZA KUSISIMUA
TUTARUDI NA ROHO ZETU?
Nchi zilizo msitari wa mbele katika Ukombozi Kusini mwa Afrika zimetendewa mambo mengi maovu na Utawala dhalimu wa Makaburu... Hata hivyo halikupata kutokea tishio zito la kutisha kama hili, ambalo linakaribia kutokea. Tukio la kutatanisha ambalo linawatoa machozi wananchi wa nchi mbalimbali za kiafrika. Wanajitokeza mashujaa na kwenda Afrika Kusini, ili kulikabiri tishio hilo lakini kila aendaye huko harudi na roho yake. Inspekta Kombora nchini Tanzania jasho linamtoka. Anawatambua na kuwakumbuka mashujaa wengi lakini anamtambua shujaa mmoja. Joram Kiango. Jambo la kusikitisha ni kwamba sasa hivi Joram Kiango ni mtumiaji mzuri ambaye sasa anatembea kutoka jiji moja hadi lingine akiwa na yule msichana wake mzuri Nuru kwa ajili ya kustarehe. Juhudi za Kombora kumsihi Joram arejee kazini hazifui dafu. Badala yake Joram anafanya maajabu mengine ambayo yanalichafua jina lake hapa nchini Tanzania na kote duniani. Wakati huo siku ambayo utawala wa makaburu umeweka ili kuachia pigo
NJAMA HADITHI YA KUSISIMUA YA UPELELEZI SURA YA TATU "Unajuwa Willy dakika ile mtu anapozaliwa pale pale anapewa huku ya kifo. Nina maana ya kusema kuwa binadamu hata aishi vipi kufa lazima atakufa. Kule kuishi baada ya kuzaliwa ina maana kuwa ile hukumu ya kifo inaahirishwa kutekelezwa.Wengine huahirishwa kwa mwezi mmoja. Hivyo mtoto anazaliwa na baada ya mwezi mmoja anakufa. Hii si ajabu maana hukumu yake ya kifo imetekelezwa baada ya mwezi mmoja. Wengine huishi hata miaka mia moja. Hii ina maana kuwa hukumu yake aliyopewa dakika alipozaliwa imetekelezwa baada ya miaka mia.Hivyo kila mtu na sehemu yake ya kuishi. Kwa hiyo kuogopa kufa ni ujinga." "Mimi sina wasiwasi, maana kifo cha namna hii, nitakuwa nimekufa kifo cha heshima", alisema Sherriff. "Okke, sasa naamini nina watu. Tokea sasa nyinyi si ndugu tena ila ni makomredi", niliwaeleza. "Kwani komredi ina maana kubwa zaidi ya ndugu?", Veronika aliuliza. "Hasa, ina maana kali zaidi.
Vifaa vya Kijeshi vilivyotia fora maonesho ya miaka 50 ya Uhuru
Gari la Jeshi likipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaye Kikwete likiwa limebeba Kifaru cha kisasa kilichofungwa makombora kwa ajili ya kutungua ndege za adui Kifaru kikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Kikwete kikiwa na mkonga wa kurusha makombora Kifari kinachotumia minyororo kwa ajili ya kukabiliana na adui kikipita mbele ya Rais Hili ni moja ya magari ya kisasa kwa ajili ya vita likipita mbele ya Rais Kikwete Gari la kisasa lenye rada kwa ajili ya askari wa Majini NAV, likipita wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
WASANII THT SASA NI GUMZO LA JIJI LA DAR ES SALAAM
HOFU
HOFU ni miongoni mwa vitabu vya hadithi za kusisimua za upelelezi kuhusu ukombozi Kusini mwa Afrika kilichoandikwa na Mwandishi Mahili wa vitabu vya Upelelezi nchini, shujaa wa Afrika Hayati A E Musiba. Kitabu hiki ni mojawapo ya vitabu vya Upelelezi vitabu vingine ni KIKOSI CHA KISASI, KUFA NA KUPONA, KIKOMO, UCHU na NJAMA, kisome kupitia NYAKASAGANI.BLOGSPOTI.COM. SEHEMU YA KWANZA PORT ELIZABETH Ilikuwa tarehe 24 Machi, baada ya mauaji ya kikatili ya waafrika 19, katika kitongoji cha Langa, karibu na Vitenhage; mji ulio karibu na ule mji wa viwanda wa Port Elizabeth, katika Jimbo la Cape Mashariki. Mauaji hayo yalikuwa yamefanyika tarehe 21 Machi, siku ya kukumbuka mauaji ya kikatili kwenye mji wa Sherpville mnamo mwaka 1960. Wakati wazalendo 69 walipouawa kikatili. Mnamo tarehe hiyo ya 24 Machi, huko mjini Port Elizabeth kulifanyika mkutano katika ofisi ya Mkuu wa Polisi mnamo saa sita usiku. Ndani ya chumba cha mkutano huo walijumuika watu ambao wamekuwa chanzo cha vilio na malalam
Komandoo wa JWTZ wafunika maadhimisho ya Uhuru Dar
NJAMA VERONIKA NA SHERRIFF II ILIKUWA saa tatu kamili niliposimama mbele ya chumba namba 208 katika ghorofa ya pili ya hoteli ya Kilimanjaro, niligonga mlango mara mbili haraka haraka, halafu nikatulia kidogo kisha nikagonga tena. Hivi ndivyo nilivyokuwa nimeelekezwa. "Karibu", nilisikia sauti kali ya juu ikitokea ndani ya nyufa za mlango. Nilifungua nikajikuta katika sebule ya chumba hiki ambamo Veronika alikuwa amevaa kaputula na sidiria tu akifanya mazoezi ya viungo. Alikuwa ameelekea upande mwingine na kunionesha mgongo na kuendelea na mazoezi yake kama kwamba hakuna mtu aliyeingia. Nilirudisha mlango, nikauegemea na kutazama jinsi binti huyu alivyokuwa akichukua mazoezi. "Karibu Willy Gamba, kaa kwenye kiti upumzike", alinielekeza bila kugeuka na huku akiendelea na mazoezi yake. Kisha akaanza kusema kana kwamba anajizungumzia yeye peke yake. "Willy Gamba anayejiita mfanyabiashara huku ni mpelelezi mashuhuri wa Afrika. Afa